MAAMUZI ALIYOCHUKUA MKE WA KEVIN HART BAADA YA MUMEWE KUCHEPUKA - teknomovies
MAAMUZI ALIYOCHUKUA MKE WA KEVIN HART BAADA YA MUMEWE KUCHEPUKA

MAAMUZI ALIYOCHUKUA MKE WA KEVIN HART BAADA YA MUMEWE KUCHEPUKA

Share This
Kwenye mitandao ya kijamii bado zinazo trend ni story zinazomuhusu Diamond Platnumz na Kevin Hart ambao mapema wiki iliyopita wamepitia kwenye majaribu ya ndoa zao.

Kevin Hart akiwa na mkewe Eniko Parrish


Diamond Platnumz amekiri kuzaa na mwanamitindo Hamissa Mobeto ambapo awali walipanga mpango huo uwe siri lakini imekuja kuwa wazi na kila shabiki akatoa mtazamo wake juu ya suala hilo. Lakini baada ya yote hayo mwenza wa Platnumz ambae ni mzazi mwenzie Zari The Boss Lady amekubali kumsamehe na kuruhusu maisha yaendelee kama kawaida.

Tukio kama hili nalo limemtokea mchekeshaji maarufu Kevin Hart ambae nae camera zilimnasa akiwa na mchepuko wakiwa ndani ya gari kwa zaidi ya dakika 20, Baada ya kunaswa nae alikiri kuwa shetani alimpitia hivyo akaomba msamaha kwa mkewe ili amsamehe na maisha yaendelee.

Sasa msamaha alioutoa mke wa Hart, Eniko Parrish upo tofauti na ule alioutoa Zari kwani Eniko amemsamehe mumewe kwa masharti ya kumpatia maneno ya siri (Password) kwenye mitandao yote anayotumia hadi Bank Account.

Usisahau kuacha Comment yako na kutufollow instagram na Tweeter @TeknoMovies

No comments:

Post a Comment

Pages