Lady Jay Dee: Aslay Mtu Mbaya. - teknomovies
Lady Jay Dee: Aslay Mtu Mbaya.

Lady Jay Dee: Aslay Mtu Mbaya.

Share This
MWANADADA nguli wa Bongo Fleva, Lady jay Dee amekiri wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa sana wa Aslay na huwa anamsikiliza mara kwa mara.

Komando Jide katika moja ya mahojiano na kituo cha Habari anasema Aslay ndio msanii anaemkosha kwa sasa sababu ana sauti nzuri ambayo huwezi kuisikia sehemu nyingine ila kwake.
“Naupenda wimbo wa Muhudumu na naweza nikakiri wazi kuwa Aslay ndio msanii ninaemkubali kwa sasa yupo vizuri,” alisema.

Aidha Jide anaetamba na wimbo wa I miss you amesema ndani ya wiki hii watu wategemee video mpya ambayo kafanya na muongozaji Justin Campos.

“Nilisafiri kwenda South Africa kufanya hiyo video na muda wowote kuanzia sasa kitu kinaweza kuachiwa,”

“Katika wimbo hizo vesi za kuchana aliandika One The Incredible, na katika korasi tulishirikiana na Domokaya na kitu kikaweza kutoka kama hivyo,” alimaliza kwa kuulezea wimbo huo.

No comments:

Post a Comment

Pages