Harmonize na Wolper bado balaa. - teknomovies
Harmonize na Wolper bado balaa.

Harmonize na Wolper bado balaa.

Share This

HALI inazidi kuwa hali hii ni baada ya majuzi msanii kutoka Wcb, Harmonize kudondosha wimbo wake mpya alioupa jina la Nimechoka ambapo kwa udadisi wa ndani ni wimbo unaonekana kumlenga mpenzi wake wa zamani Jackline Wolper.

SOMA PIA: DOWNLOAD HAPA HARMONIZE-NISHACHOKA

Kuonesha kwamba yeye Wolper si wa mchezo mchezo,kupitia akaunti yake ya Instagram alipost dongo zito kuelekea kwa Harmonize huku akizidi kumtuhumu yeye kuwa ndiye mdanganyifu wa mapenzi na si kama jinsi Harmonize anavyodai, na baadae akafuta post hizo.

Baada ya dongo hilo Harmonize ameamua kujibu nae katika akaunti yake ya Instagram, ambapo alipost video fupi akiwa na mpenzi wake mpya na kuandika maneno kadhaa.
“Vipi kwani??Mbona nasikia mtaa wa 3 povu kwani katajwa mtu? Meseji ikishafikaga..Ukweli unaumaga..??#Nimechoka mwambie tena anaejifanya anakujua sana…Pambana na Huba lako”

Baada ya mapovu ya wote wawili juhudi za kuwatafuta kila mmoja ili kuweza kuelezea jambo hilo linaloendelea zimegonga mwamba sababu hakuna anaepokea simu kujibu juu ya mapovu hayo.

Tazama hapa Chini Post ya Harmonize akiwa na mpenzi wake Sarah.

No comments:

Post a Comment

Pages