Flaviana Matata Mniache Na Wembamba Wangu - teknomovies
Flaviana Matata Mniache Na Wembamba Wangu

Flaviana Matata Mniache Na Wembamba Wangu

Share This
MWANAMITINDO na pia mrembo wetu wa nguvu ambae kazi zake nyingi anazifanya kwa Madiba “South Africa” nae majuzi aliachia povu zito kwa watu ambao wamekua wakimsema kua anazidi kua mwembamba.

Katika akaunti zake katika mitandao ya kijamii, watu wamekua wakimsema kua mwanadada huyo anazidi kua mwembamba na hivyo inabidi awe anakula na si kujinyima msosi ili kuzidi kuuweka mwili wake kimwanamitindo zaidi.

Flaviana aliandika (Imetafsiriwa) “ Kiukweli watu inabidi wajifunze kudili na mambo yao na kujali mambo ya maana zaidi. Nimechoka na ushauri wa ajabu eti “NAHITAJI KULA” mnaonipa kwenye komenti, kwani nani ambae kawaambia mi sili? Watu wengine tupo hivi hivi na tunajivunia. Nawaombeni mtunze nguvu zenu na hayo maoni yenu pia. Nina furaha kwa mwili wangu ulivyo na ndicho nachojali,” alimaliza kwa namna hiyo.

Tazama Chini Post Original alichoandika.

No comments:

Post a Comment

Pages