DAXX KUJA NA KIPINDI CHA TV - teknomovies
DAXX KUJA NA KIPINDI CHA TV

DAXX KUJA NA KIPINDI CHA TV

Share This
Habari njema ikufikie wewe mpenzi wa movie kwamba mkali wako Frank Daxx ambae anakuletea uchambuzi wa movie mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii sasa utarajie kuona uchambuzi huo na stori za mastar wa movie kwenye TV kupitia kipindi cha 'The Action'.


Kipindi hiki kitakujia kila weekend kwenye channel ya DM Online TV na cha kufanya sasa nenda You Tube subscribe channel ya DM Online TV ili uwe wa kwanza kushuhudia ujio huu wa mkali wako Daxx.

Mtandao wa Teknomovies umefanya mahojiano na Frank Daxx kujua namna ya kipindi kitakavyokuwa na mahojiano yetu yalikuwa hivi.

Teknomovies : Oya Daxx niaje mzee?

Frank Daxx   :  Fresh man harakati zinasonga

Teknomovies :   Ndio jambo la msingi hilo, Ebhana daxx nimeona nikutafute kwa ajili ya kuzungumzia ujio wa kipindi chako kwenye TV.

Frank Daxx   :   Yeah ujue hiii issue nilikuwa naiandaa kimya kimya ila imefika time ya kuwaambia mashabiki zangu na wale wapenzi wa movie kwa ujumla kuwa Daxx nimewaandalia kitu kikubwa, Nimeamua kuja na kipindi cha TV ambacho ni mahsusi kwa movie tu na kitakuwa kwenye Youtube kwenye channel ya DM Online TV.

Teknomovies  : Ni vitu gani vimo ndani ya hicho kipindi?

Frank Daxx     : Swali zuri sana....!!! Kwa ujumla kipindi kimeshiba mana ndani yake kutakuwa na Stori zinazowahusu mastar wa movie, Teknolojia zinazotumika kwenye movie, tutaona pia namna ya location zilivyo na behind the scene kwenye movie yani niseme tu kwamba ni Package ya Kutosha.

Teknomovies :  Neno la mwisho la kuwaambia mashabiki

Frank Daxx   :   Kwanza nishukuru kwa interview hii leo nimepatikana....(Haaahaaahaa) Anyway kwa ujumla nawashukuru sana mashabiki wangu mana wao ndo wamenisukuma kufanya hii kitu, wamekuwa na mimi kwa wakati wote hivyo ni jukumu langu kuhakikisha nawahabarisha kila kitu kutoka kwenye kiwanda cha movie, cha kufanya subscribe Youtube Channel ya DM Online TV ili uwe wa kwanza kushuhudia kipindi cha The Action.

Yes hayo yalikuwa mahojiano kati ya mtandao wa Teknomovies na Daxx na hii ndio Trailer ya kipindi chenyewe cha The Action....Don't Miss.




No comments:

Post a Comment

Pages