Ruksa Kubisha Katika Hili. - teknomovies
Ruksa Kubisha Katika Hili.

Ruksa Kubisha Katika Hili.

Share This
  Ni kawaida sana kukuta mtu kama Harmorapa ametusua maisha kuliko Nikki Wa Pili, Na ukifuatilia kiundani utagundua kwamba huyu Harmorapa alifanikiwa kwa kutumia mawazo ya Nikki Wa Pili.

Kuna vitu vingi ambavyo mtu wa aina ya Harmorapa anaweza kuvifanya vikamtoa kimaisha wakati mtu wa aina ya Nikki Wa Pili hawezi kuvifanya kwasababu ya status yake ya usomi.

 Ndo maana matajiri wa dunia sio watu wenye Masters au PhDs, hao wenye PhDs wengi wanaishia kupata pesa ya mbuzi na mchele, kigari kimoja au viwili, na kuajiriwa na hao wasio na hizo PhDs!

Mfano rahisi: Mpe shilingi laki 1 mtu aliyeishia darasa la 7 au form 4 halaf mpe pia laki moja mtu aliyehitimu Chuo Kikuu. Ukija kuonana nao miezi miwili baadae utakuta yule darasa la 7 anamiliki genge la kuuza matunda na mtaji wake ushaongezeka umekua laki mbili..

Wakati yule wa Chuo Kikuu ile laki moja alienda kununua jeans au Kiatu kikali, au aliimalizia kwenye vifurushi vya Internet na ana bidii kweli kuitusi serikali mitandaoni kwamba haitoi ajira! 

Mwandishi@DarasaHuria

Pages