BONGO MOVIES MJIFUNZE KIUMENI#MAKALA. - teknomovies
BONGO MOVIES MJIFUNZE KIUMENI#MAKALA.

BONGO MOVIES MJIFUNZE KIUMENI#MAKALA.

Share This

Kwa Mara Ya Kwanza Kabisa Nilianza Kuona Tangazo Kupitia Akaunti Ya Rafiki Yangu Instagram Akipost Taarifa Mbalimbali Kuhusu Ujio Wa Movie Hii Ya KIUMENI.

Nilipoitazama vizuri Cover Nilipata Kuona Kitu Tofauti Sana Tofauti Na Cover Nyingi Sana Za Bongo Movies... Na Zaidi Nilipoona Hata Washiriki.

Macho Yangu Yalitua Kwa Hili Jina ERNEST NAPOLEON... Si mara ya kwanza Kuona Jina Hilo Na Nilipojaribu Kukumbuka Vyema... Jina Hili Lilikuja Kichwani GOING TO BONGO.

Yeah Hiyo Ni Movie Ambayo Naikumbuka Vyema Sana Kitu Kama Ilitoka Mwaka 2015 Na Ilipata Sifa Lukuki Kwa Kuoneshwa Kwenye Baadhi Ya Cinema Nchi Nyingi Duniani.

Nafikiri Hii Ndo Movie Ambayo Ilimtangaza Vizuri Huyu Jamaa ERNEST NAPOLEON Ki Dunia Na Hata Kwa Tanzania Pia Katika Sekta Ya Movie.


Kuna Vitu vichache Ambavyo Ningependa Kuviongelea inshort Kuna Vitu vingi Sana Bongo. movies Inabidi Wajifunze Hapa.. Kivipi Ni Hivi..

Cha Kwanza, Kuzindua Movie Katika Ma Cinemas.
   Kwangu mimi sababu sio mfwatiliaji sana wa Bongo Movies Naikumbuka Filamu Moja Ambayo Ilitangazwa Sana Nayo...na Walikua wamecheza Ndani Kanumba na Monalisa kama ndo ma leading role..

 Filamu hiyo ilikua imeandaliwa na makampuni ya nje.. Nakumbuka Filamu Hiyo Ilizinduliwa Kwenye Cinema Kama Sasa KIUMENI na Hata GOING TO BONGO Ilivyofanyika.. Kibongo Bongo ni nadra sana kusikia filamu zikizinduliwa Katika Cinemas Sijajua Tatizo Ni Nini?! Mara Nyingi naona tu mchongoo huo ushatoka.


Kwa nchi za nje, system ya kuachia movie mara nyingi huwa ni kwenye cinemas Mbalimbali na hapo ndo pesa huanza kukusanywa kabla ya kupelekwa sokoni.

Kitu cha pili, ambacho bongo movie wajifunze ni kufanya usahihi vizuri katika selection za soundtracks... Kwa wenzetu swala la selection ya soundtracks inafanywa kwa utafiti mzuri utaoendana na movie... Mfano movie kama FAST & FURIOUS7 Hata pia SUICIDE SQUAD... na Pia Fast 8  ni movies ambazo wasanii walikusanywa baadhi na kutunga nyimbo mahususi kwaajili ya movies hizo.. Na hua inatoka album ambayo huuzwa tofauti na movie.. Najua wengi mnaukumbuka wimbo wa Wiz Khalifa see you again aight...

Katika movie ya KIUMENI Nimepata Taarifa kua Wamezingatia vyema sana katika swala zima la soundtracks ambapo Mzigo wa music alisimamia P funk majani Na wengi tunaujua ubora wa P katika production ya nyimbo bora na zenye Quality bora pia... Na nyimbo maalumu za movie zimefanywa hapo.
 Hii issue katika bongo movies siioni kabisa sijui ndo kubana matumizi i don't know?!

Tunatamani kuona movie za Bongo hazioneshwi Tz tu... Zinaoneshwa maeneo mengi ya dunia.. Ila kufikia huko mfumo wetu inabidi ubadilike sana.

Kwanza tufanye mgawanyo wa kazi vizuri, tatizo kubwa kwetu ni watendaji wa kazi katika kuandaa movie huwa ni wachache sana na wengi huwa wana cover nafasi nyingi ambazo kwangu naona kila mmoja kwanini asisimame eneo lake... Mfano utakuta mtu mmoja ni Director, producer, actor, script writer...

Ni kweli kuna baadhi ya movie hata wenzetu huwa hivyo lakini asilimia kubwa wenzetu huweka mgawanyo mzuri bila kuingiliana katika kazi... Kuna mengi natamani nieleze hapa.. Ila nitaandaa makala Maalumu kuhusu ndugu zetu hawa wa Bongo movie...ila kwa hili naomba watu waanze kujifunza kupitia movie hii ya Kiumeni.

Kesho Tarehe 17 ndo itaachiwa rasmi pale mlimani city katika cinema.. Na kwa week nzima itaoneshwa hapo.. Ko jipatie tiketi yako mapema ili kuweza kufaidi vipaji toka Tanzania..


Pages