TRAVELMATE: BEGI LINALOTEMBEA LENYEWE KUMFUATA MMILIKI WAKE - teknomovies
TRAVELMATE: BEGI LINALOTEMBEA LENYEWE KUMFUATA MMILIKI WAKE

TRAVELMATE: BEGI LINALOTEMBEA LENYEWE KUMFUATA MMILIKI WAKE

Share This
Sote tunafahamu adha inayopatikana katika ubebaji wa Begi au mabegi pale tunaposafiri kuelekea katika kituo aidha cha Mabasi, Treni au Ndege.


Hali hiyo sasa inakaribia kuondoka kabisa baada ya kufanyika mageuzi makubwa ya kiteknolojia kwa kuundwa begi la kisasa.

Travelmate ndio begi la kwanza duniani ambalo linatembea lenyewe bila kubebwa kuelekea kule ambapo muhusika wa begi anapoelekea.

Begi hilo la aina yake linalofanya safari iwe rahisi lilizinduliwa na kampuni ya Travemate mwaka 2016 mwezi Oktoba.  

Ni begi linalotumia Teknolojia ambayo hutakuwa na kazi ya kulibeba bali litakuwa linakufuata popote uendapo.

Ili liweze kufanya kazi vizuri na kumfuata mwenye begi limeunganishwa na simu kupitia GPS ili kuweza kumfatilia mmiliki wake kwa usahihi zaidi. Popote utakapoliweka utaweza kulifuatilia
kupitia GPS.

Begi hilo linaweza kutembea kwa vertically (wima) na horizontally (usawa) na unaweza kuongeza mzigo juu yake na likaendelea kutembea bila ya taabu yoyote.

Pia Linaweza kupita popote bila shida yoyote. Linarekebisha mwendo wake ili liwe  nyuma yako kidogo. Kasi yake ni maili 6.75 kwa saa (sawa na 10.8km kwa saa) Begi hilo linatumia Battery ambalo unaweza kulitoa. 

Unaweza kulichaji kwa njia ya wireless au kwa njia USB. Battery yake inakaa na Chaji kwa masaa 4 likiwa linatumika. Na bila ya kutumika chaji inakaa kwa masaa 100. Unaweza kuweka LOCK kwa kutumia fingerprint.    


Begi hilo linalozalishwa Marekani linapatikana kwa rangi mbalimbali, na Bei yake linaanzia dola 399. 
Bei hilo linatarajiwa kuuzwa mwezi june mwaka huu tayari milango ya kuweka oda ipo wazi.


TAZAMA HAPA CHINI VIDEO.




Source : Muungwana Blog



No comments:

Post a Comment

Pages