Kutokana na mashairi ambayo yalikuwa yakiishambulia
kambi pinzani kama mawaki (hawajui kitu) kina Dre nao wakawa wanarudisha
makombora kuonesha ni namna gani wanajua game ya Hip Hop….Hapo ikawa katika
kila showa lazima wasanii watoke pande zote yani Esat na West na hapo Free
Style battle zikawa zinachukua nafasi kwa kiasi kikubwa.
Endelea………….
Ukiachilia sababu za kurap na diss track kutoka
pande zote, Pia kuna sababu ambazo zipo nyuma ya pazia zilizochochea uhasama
huu kukua kati ya mwaka 1994 hadi 1997. Miongoni mwa sababu hizo ni ushindani
uliopo katika Record Label zao, namna vyombo vya habari vinavyowapa airtime
(Media Coverage) , utamaduni lakini pia wasanii wawili ambao wapo katika pande
hizo wenye style kali za mashairi (Tupac & Notorious).
Ikumbukwe hawa jamaa wawili walikuwa marafiki kabla
ya kuwa na beef, walikuwa wakifanya show pamoja, wakila bata pamoja na
kujifunza maarifa kutoka kwa wengine juu ya game ya hip hop. Haya yote yalikuja
kuvurugika baada ya 2Pac kupigwa risasi akiwa studio katika jiji la New York na
kwa bahati mbaya wakati tukio hili linatokea Biggie na P Diddy walikuwepo eneno
hilo. Zikawepo nadharia nyingi juu ya tukio hilo lakini 2Pac alipeleka shutuma
moja kwa moja kwa rafiki yake Biggie Nototrious kuwa alipanga amuue na hapo
urafiki ukayeyuka kama moshi angani.
2Pac alimtuhumu Biggie kuwa alichonga mchongo wote
huo na kwa kipindi hiko wawili hao walishakuwa maarufu katika ardhi ya Marekani,
aliamini kuwa mwenzake alifanya hivyo ili yeye abaki mwenyewe na aendelee
kutawala game ya hip hop nchini Marekani na duniani kwa ujumla.
Baada ya tukio hilo 2Pac aliswekwa lupango na baada
ya kutoka alitumia mbinu zake zote za kimuziki kumshambulia Biggie na katika
kipindi hiko ndipo alipotengeneza Diss Track ya “Hit em Up” na hiyo ikamvuruga kabisa hasimu
wake.
Tupac alihakikisha anaharibu kila kitu cha biggie
sokoni, kuanzia kwenye mauzo hadi kwenye record label zake. Tukio linguine alilolifanya
ni kuchukua picha yake na ya mke wa Biggie kisha akasema alilala nae, hii
ilimuharibia sifa kabisa Biggie kwenye game na kama unavyojua ishu ya kumegewa
inavyouma.
Pamoja na visanga vyote hivyo Biggie hakutoa diss
Track kujibu mapigo wala hakujibu lolote juu ya kile kilichoendelea aliendelea
na mishe zake kama kawaida mpaka baadae alipokuja kuachia ngoma “Who shot ya” na
hii aliichia baada ya kifo cha Tupaxc.
Itaendelea………….
Usisahau kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies na pia Ku Subscribe youtube channel ya DM Online Tv