Ukumbuke ni vichwa viwili tu ambavyo vilitazamwa kwa
jicho la ushindani kwenye game ambao ni Tupac na Biggie Notorious. Biggie akawa
amebaki mwenyewe, ingawa yeye binafsi aliona hiyo ndo time ya kung’aa kwenye
ramani kwani pamoja ya kuwa na beef na Tupac lakini dunia ilikuwa inamuelewa
zaidi Tupac kuliko yeye, wajibu wake uliokuwa mbele ni kuhakikisha na yeye
anajenga umaarufu kama wa Tupac au pengine zaidi.
Endelea……..
Pamoja ya kuwa Harakati za muziki zilikuwa
zikiendelea lakini ukweli ni kwamba kila mmoja alikuwa na wasi wasi juu ya
mustakabali wa maisha yake ya mbeleni. Kila mtu hakujua nini kingefuata. Kibaya
zaidi ni kwamba Biggie aliachia Diss Track kwenda kwa Tupac aliyoipa jina la
“Who Shot Ya” ambapo lengo lake ni kujihami na sekeseke la kuhusishwa na mauaji
hayo.
West Coast Side ilibaki na wasanii wakubwa watatu
ambao ni Snoop Doggy, Easy E na Dr Dre upande huu haukua na nguvu tena kwani
waliobaki wote si watu wa ma beef au watu wanaopenda figisu figisu huku Upande
wa East Coast Side chini ya Record label ya Bad Boyz iliyokuwa ikimilikiwa na
Puff Daddy tayari walikuwepo wakali kadhaa akiwemo Jay Z na Notorious Mwenyewe
ambao hawa walikuwa wanang’aa kupita maelezo. Coverage ya media yote ikawa East
Coast Side, Interview nyingi wakawa wanapewa East Coast Side.
Maisha yakawa yanasonga lakini mke wa Biggie Faith
Evans (ambae aliimbwa na Tupac kwenye wimbo wa Het Em Up) alikuwa akiogopa sana
kwani baadhi ya watu walidhani aliyepanga mauaji ya Tupac ni mumewe . Hata
hivyo Biggie hakuwa na kibali cha muda mrefu cha kuvuta pumzi kwenye uso wa
dunia kwani miezi 6 baadae alidunguliwa na yeye kwa risasi ambazo zilichukua
uhai wake.
Tukio la kupigwa risasi lilifanywa tarehe 8 march
1997 siku ambayo Biggie na yeye alikuwa akitoka kwenye party huko Petersen
Automotive Museum, akiwa amekaa kiti cha mbele kabisa katika gari aina ya SUV
Chevrolet ambapo mdunguaji alitegea gari isimame ili ampate vizuri. Baada ya
gari kusimama mlengaji alifyatua risasi mara nne ambazo zote zilimpata Biggie
Notorious. Alikimbizwa katika Hospitali ya Cedars- Sinai lakini
ilipofikia saa 7: 00 usiku Biggie aliaga dunia.
Itaendelea……
Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.