WIKI kadhaa zilizopita msanii mkongwe Chidi Benz alisikika
akisema kuwa yupo kwenye mipango ya kufanya kolabo yake na Tupac. Alipoulizwa
zaidi kwamba Tupac yuko wapi,kwa majibu yake alisema kuwa yupo Cuba.
Kutokana na kauli hiyo wengi waliichukua kama msanii huyo
ameanza kuchanganyikiwa na kuanza tena kurudia matumizi ya unga pasipo kujua
sio yeye pekee ambae anaamini Tupac yupo hai na sehemu wanayoamini kuwa yupo
Cuba.
Nao vipi tunaweza kusema ni machizi? Ukiachana na hicho
wanachokiamini pia wana sababu nzito ambazo huzitumia katika kuamini kwao.
Katika makala hii nimekuandalia baadhi ya sababu kadhaa ambazo
zinafanya kifo cha Tupac kionekane kama ni uongo uongo na kuwa mshikaji yupo
sehemu Fulani anakula kuku kwa mrija huku akiendelea kutucheki na wasanii wetu.
Mwili wake baada ya kufa.
Baada ya Tupac kupigwa risasi na
kufariki mwaka 1996 mwili wake ulichofanyiwa ni kama wahindi wanavyofanya
ulichomwa moto lakini baada ya tukio haukuwahi kuonekana tena.
Kiongozi wa lebo ya Death Row ambae siku ya kupigwa risasi kwa
Tupac alikuwa nae pamoja , Suge Knight anasema “ mtu ambae alitakiwa kuchoma
mwili wa tupac nilimpatia kiasi cha dola milioni tatu toka kwangu tena keshi,
lakini kitu ninachokijua baada ya hapo ni sikuwahi msikia tena huyo jamaa au
kumuona nilisikia alistaafu na kuondoka,”
“Huwa najiuliza Tupac kwa hili ni kweli alikufa, sasa yuko
wapi,” aliongeza.
2.
Picha yake ya mwisho.
Tupac alipigwa risasi Septemba 7 mwaka 1996 huko Las Vegas. Lakini
cha kushangaza kidogo picha yake ya mwisho iliyopatikana akiwa pamoja na Suge
Knight ilikuwa imepigwa septemba 8 na kuzidi kuleta sintofahamu katika hilo
suala.
3. Makaveli
Katika albamu yake ya The Don Killumunati:The 7 Day Theory
iliachiwa huku Tupac akijiita Makaveli.
Jina hilo alianza kujiita Pac likitokana na mwanafalsafa
maarufu kutoka Italia ambae alikuwa akiamini katika kuigiza kifo kama njia ya
kumpiga adui yako katika vita. Kimbembe ni kuwa picha ya albamu ilimuonesha
rapa huyo akiwa katika msalaba na akiamini kuwa baada ya kifo chake angefufuka
baada ya siku saba.
Na pia ukichukua neno Makaveli,kama ukilipangua unapata “Am alive.K.”
Hapo ndio utata uzidi kwamba jamaa vipi kwani.
4. Mistari Yake.
Kuna baadhi ya mistari yake ambayo
iligusia kuhusu kifo chake hata kabla tukio halijatokea.
Katika wimbo wa “Ain’t hard 2
find” kuna mistari anasema “I heard rumor that I died ,murdered in cold blood
traumatized/pictures of me in my final states-you know Mama cried . but that
was fiction,some coward got the story twisted,” kwa tafsiri ya kwamba “Nimesikia
watu wakiongea kwamba nimekufa,nimeuwawa kikatili kwa kuogofya,najiona katika
nyakati zangu za mwisho na najua Mama unalia lakini hayo ni maigizo waoga
wamegeuza stori,” hapo vipi kwanini watu wasiwe na mashaka na jamaa kwamba yupo
hai?
Hapa ndio watu hukosa zaidi
majibu, baada ya kifo chake Albamu za Tupac tisa zimeweza kuachiwa na baada ya
kifo umaarufu wake ulizidi maradufu. Swali linakuja alipata muda gani kurekodi nyimbo
zote hizo za kuweza kukaa katika albamu tisa?
Hapa labda ndio muanze kumuomba
ladhi Chid Benz. Watu wanaamini kwamba dizaini Fulani yupo Cuba kisa ni kuwa
,Pac alikuwa na ukaribu sana na mwanaharakati Assata Shakur ambae inasemekana
kuwa alikimbilia nchini Cuba.
Mwanamke huyo wa nguuv ambae
mpaka sasa endapo atakanyaga ardhi ya Marekani basi hukumu yake itakuwa ni kifo
hivyo aliamua kukimbilia Cuba ambako mpaka leo anaishi huko.
Kwa maana hiyo watu wanahisi itakuwa
aliamua kuacha seke seke huku na kwenda kuungana na mwanaharakati huyo.
7 Video
zake.
Katika video ya Toss it Up Tupac
anaonekana akiwa amevaa snika ambazo hazikuwepo kipindi anakufa.
Pia kuna wanaosema katika video ya
Live and Die in La wakati Tupac anaruka katika gari anaonekana akiwa amevaa
snika za Michael Jordan ambazo hazikuwepo kwa kipindi hicho.
Vyanzo:Oxygen.com na mitandao mingine
Vyanzo:Oxygen.com na mitandao mingine
No comments:
Post a Comment