Ni ukweli kabisa
hakuna njia maalum ili kuepuka baadhi ya
hatari katika maisha yetu ya kila siku, lakini tunaweza kufanya hatari hizo
zipungue kutokana na mienendo yetu. Hii hapa ni list ya miji mitano hatari
zaidi duniani.
5. Kabul, Afghanistan
Afghanistan ni
nchi yenye vita, wakati wote majeshi ya magharibi yamepiga kambi hapo
kusambaratisha vikosi vya kigaidi kama Al-Shabaab. Kujiua kwa mabomu (Kujitoa
mhanga) ni kawaida sana kusikia kwani ni kama desturi.
Hili ni eneo
hatari zaidi katika mataifa ya Asia.
Kabul Afghanistan |
4. Cape Town,
South Africa
Hili nalo ni
moja ya eneo hatario zaidi duniani ingawa kwa kiasi kikubwa idadi ya vitendo
vya kihalifu imepungua, sababu kuu inayofanya eneo hili kuwa na hatari zaidi ni
kutokana na kuwepo kwa idadi ya wahamiaji wanaoingia mjini humo. Usishangae
kufika Cape Town na kukuta dawa za
kulevya zikiuzwa kama njugu kwani ndio tabia ya mji huo na inakadiriwa ni zaidi
ya 14% ya vijana huongezeka kila mwaka katika matumizi ya dawa za kulevya.
Vipo vikundi
vinavyojihusisha na uhalifu wa kuvunja milango na kuingia majumbani kisha
kupora na muda mwingine huua kabisa.
3. Caracas, Venezuela
Kifo cha Rais
Hugo Chavez mwaka 2013 imeonekana kama ni matokeo ya kuongezeka kwa uasi katika
mji mkuu wa nchi hiyo.
Wananchi mara nyingi wanaingia mtaani kuandamana na
kushinikiza serikali iliyopo idhibiti masuala ya rushwa pia huripotiwa vifo vya
mara kwwa mara. Vikundi vya kihalifu huongezeka siku hadi siku hali
inayopelekea ukosefu wa amani katika nchi hiyo.
2. San Pedro
Sula, Honduras
Hakuna shaka
kwamba Honduras inapokea wageni wengi wa kitalii kutokana na hali yake ya
kuvutia ya kitropiki. Uhalifu unafanyika sana katika maeneo ya San Pedro Sula,
na watalii mara nyingi ni waathirika wa utekaji nyara na uhalifu mwingine wa
kifedha na mara nyingi wanauawa. San Pedro Sula ina bahati mbaya ya kuwa mji
mkuu unaoongoza kwa mauaji dunia nzima.
1 1. Aleppo,
Syria
Dunia nzima
inafahamu hali ya kisiasa nchini Syria, mapigano ya kijeshi ni ya kawaida.
Wakazi wengi wa Aleppo wanaishi kwa hofu kama wakimbizi na wamekimbilia juu ya
mpaka katika nchi jirani ya Uturuki. Maisha ya mapigano ni maisha ya kila siku
na ni magumu zaidi kutokana na ukosefu
wa mahitaji ya msingi kama vile umeme na maji ambavyo mara kwa mara huvurugika
au kukatwa kabisa.
Usisahau kuacha comment yako na kutufollow Instagram na Twitter @TeknoMovies
No comments:
Post a Comment