Tunajua kabisa kuwa hapo awali takwimu zilikua zinaonyesha Samsung akiwa namba moja, Apple namba mbili na wa tatu akiwa ni Huawei.
Hilo limebadilika kwa sasa, Huawei anashikilia namba mbili kutokana na asilimia ya mauzo aliyoyafanya kwa mwezi juni na julai ambayo yalizidi kampuni la Apple.
Taarifa zilizopo zinasema kuwa kampuni imeweza kufikia katika sehemu hiyo baada ya kuwekeza zaidi katika utafiti na uboreshaji na pia hata katika kukuza huduma za masoko yake. mfano mzuri wa hili ni pale kampuni ilipotoa simu ya toleo maalum la KFC.
Lakini mambo yanaweza yakawa ni mazuri kwa Huawei lakini sio mazuri sana kwani soko lake kuu ambalo ni tegemezi ni lile soka la nyumbani (China) nje ya hapo kuna soko dogo sana.
Jambo hili inabidi libadilike kwani kutegemea soko moja sio jambo zuri kabisa katika biashara. hivyo basi inabidi jitihada zifanyike na hatimaye wapate soko lingine katika moja ya masoko makubwa
Japokuwa huawei imekua namba mbili lakini hakuna simu ambayo inaipaisha katika nafasi hiyo. Mpaka sasa simu ambayo ni maarufu imekua ni ile kutoka Apple yaani iPhone 7 na iPhone 7 Plus. Simu za Android ambazo zinaongoza kwa mauzo duniani ni Samsung Galaxy S8 na S8 Plus.
Kwa haraka haraka tuu ukiangalia katika listi hizo mbili hakuna mahali jina la Huawei lilipotokea, hivyo basi wana kibarua kikubwa sana kukaa katika namba mbili hiyo hiyo kwa kipindi cha muda mrefu.
Taarifa za mauzo kwa kampuni hizo tatu |
Pengine Apple wakiweka sokoni toleo lao lingine ndio itakua mwisho wao na kurudi katika namba yao.
Ningependa kusikia kutoka kwako, nini maoni yako juu ya hili? je huawei wamejitahidi, wape neno moja hapo chini sehemu ya comment.
No comments:
Post a Comment