FAHAMU UANDAAJI WA FILAMU ULIPOANZIA. - teknomovies
    FAHAMU UANDAAJI WA FILAMU ULIPOANZIA.

FAHAMU UANDAAJI WA FILAMU ULIPOANZIA.

Share This


           Duniani kuna kila aina ya burudani na burudani hizo zimejizolea mashabiki wengi. Kwa mfano muziki una mashabiki wake, mpira una mashabiki halikadhalika na filamu (movie) pia ina mashabiki wengi na kila mojawapo ina historia yake namna ilivyoanza mpaka sasa tunaposikiliza au tunapotazama tuka enjoy kile tunachosikiliza au tunachokiona.

Mkali wangu unaefuatilia mtandao wa teknomovies leo nimeona nikufahamishe tu namna filamu zilivyoanza, kuanzia utengenezaji wake, vifaa vilivyokuwa vikitumika pamoja location mbalimbali zilizokuwa zikitumika.

Kwanza kabisa sote tunafahamu kuwa chombo kikuu cha utengenezaji wa filamu ni kamera, yani unaweza kuwa na script, location, characters na vitu vyote lakini kama hauna cameras basi huwezi kutengeneza filamu, kwa maana hiyo huwezi kuzungumzia filamu na kuacha kamera (ni vitu vinavyolandana). Kwa mantiki hiyo utengenezaji wa filamu umechukua nafasi baada ya muunganiko wa fikra za watu tofauti.

Historia ya filamu ilianza mwishoni mwa miaka ya 1800 na hii ni baada ya kugundulika kwa kamera jongofu (motion/moving camera) kutoka kwenye kampuni moja ya production. Kabla ya muda huo kamera zilikuwepo ila zilikuwa na uwezo wa kuchukua picha mgando tu (Still Picture)

Camera ya kwanza kuchukua picha jongofu (Mortolized Camera)
Edward Muybridge(1830-1904) alikuwa mpiga picha mashuhuri sana na ukisema yeye ndie mtu wa kwanza kabisa kuwa na ‘idea’ ya filamu utakuwa hujakosea. 

JARIBIO LAKE LA KUTENGENEZA FILAMU.

Mwaka 1877 Edward alifanya jaribio la kutengeneza filamu (kumbuka kipindi hiki hakukuwa na motion camera). Alitumia kamera zake mbili kumpiga picha farasi aliyekuwa anatembea na farasi aliyekuwa anakimbia. Alipiga picha nyingi kuanzia farasi anaponyanyua mguu mpaka anavyokimbia. Baada ya kufanya hivyo akaziunganisha kwa mtitiriko sawia, akawa anazizungusha kufuatia mtitiriko ule, kwa hiyo mtu alikuwa akitazama namna zinavyozunguka basi anaona kama farasi anaeanza kutembea mpaka kukimbia, mfumo huu aliupa jina la “Zoopraxiscope”.

Baada ya jaribio lake hili wataalamu wengine wakaiboresha ‘idea’ ya Edward na ndipo David Griffith akagundua camera yenye uwezo wa kuchukua ‘motion picture’ lakini ikawa na uwezo wa kurekodi filamu yenye urefu wa dakika 1 tu.

Mwaka 1899 ikavumbuliwa kamera yenye uwezo wa kuchukua filamu yenye urefu kiasi lakini bila sauti, rangi na picha zikiwa kasi ‘chase film’(rejea movie za Charlie Chaplin) na filamu ya kwanza kutengenezwa ilikuwa ni story ya kweli kuhusu uvamizi kwenye treni na ikapewa jina la “Great Train Robbery”.
The Great Train Robbery Film
Filamu ya kwanza ndefu ilitengenezwa mwaka 1906 nchini Australia na ikapewa jina la “The Nickeledon” .

Kuanzia miaka ya 1920 teknolojia mpya ya filamu ikavumbuliwa na ikashika chati katika utengenzaji wa filamu ikiwemo kutumia taa sehemu za giza, kutumia rangi, kumove na kamera.

 Baada ya hapo ndipo wamarekani wakaanzisha Hollywood chini ya muasisi Griffith kisha teknolojia nyingine zikavumbuliwa na hadi leo tuna enjoy tukitazama movie.

Ni hayo tu kwa leo mkali wangu usisahau kutufuata instagram na Tweeter @TeknoMovie, Pia usisahau kutuachia comment yako.

No comments:

Post a Comment

Pages