WhatsApp Waongeza Uwezo Mwingine Tena - teknomovies
WhatsApp Waongeza Uwezo Mwingine Tena

WhatsApp Waongeza Uwezo Mwingine Tena

Share This
kuchati whatsapp

Unataka kutuma mafaili ya aina yeyote kupitia WhatsApp? Toleo jipya la WhatsApp linalosambaa kwa watumiaji wake linamuwezesha mtumiaji kutuma faili la aina yeyote kwenda kwa mtu mwingine.

Toleo hilo jipya limeanza kupatikana kwa watumiaji wa simu za Android na iOS kupitia masoko yake ya apps na tumefanikiwa kujaribu kutumia na ni kweli mabadiliko hayo yamekuja.

Tokea mwaka jana waliwezesha utumaji wa mafaili ya mfumo wa PDF, .doc, .txt, .csv na .xls ila kuanzia sasa utaweza kutuma mafaili ya aina yeyote.

Jinsi ya kutuma mafaili ya aina yeyote kupitia WhatsApp

> Katika eneo la kuchati bofya alama ya kutuma faili, kisha bofya Document.

Kutuma Mafaili ya Aina Yeyote kupitia WhatsApp
Kutuma mafaili aina yoyote kwa whatsapp
                
> Kuanzia sasa badala ya kuona mafaili yale ya txt, pdf na mangine kama hayo kama zamani kuanzia sasa kama unatumia toleo jipya basi utaweza kuona na mafaili ya mifumo mingine pia. Bofya na kutuma.
              Kutuma Mafaili ya Aina Yeyote kupitia WhatsApp


Ila bado kiwango cha ukubwa wa mafaili unayoweza kutuma kipo chini, kwa kutumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) utaweza kutuma hadi faili la ukubwa wa MB 64, kwa Android ukubwa wa MB 100 wakati kwa watumiaji wa iOS (iPhone) wao wataweza kutuma hadi faili la ukubwa wa MB 128.
PITIA HAPA PIA: NYUMA YA CAMERA FAST 8

         Ukilinganisha kwenye app zingine: Kwenye app ya kuchati ya Telegram mtumiaji anaweza kutuma hadi faili la ukubwa wa GB 1.5.

Vipi je umepokeaje habari hizi nzuri kwa watumiaji wa app ya WhatsApp? Kumbuka kusambaza habari hii nzuri kwenye makundi ya WhatsApp kwa wengine kwa kutumia huduma yetu ya kushare.

Chanzo: mtandao wa Teknokona

Pages