Ed Sheeran Afuta Akaunti Yake Ya Twitter - teknomovies
Ed Sheeran Afuta Akaunti Yake Ya Twitter

Ed Sheeran Afuta Akaunti Yake Ya Twitter

Share This
Jumatatu hii mwanamuziki Ed Sheeran amefuta akaunti yake ya Twitter, katika Sababu zisizojulikana.

Kitendo hicho kimetokea baada ya Ed kutokea kama mgeni mwarikwa katika Series ya Game of thrones ambayo ilipata maoni mazuri kutoka kwa mashabiki na baadhi wakiiponda katika ujio wake wa Msimu wa 7.

Baadhi ya wadau wanahisi Ed Sheeran kafanya hicho kitendo kutokana na baadhi ya maoni ya mashabiki ambao wamekua wakimponda mwanamuziki huyo na wengine wanahisi ni kitendo ambacho kaamua yeye mwenyewe kukifanya kwa sababu zake.

Katika instagram chakushangaza alionekana akiwa bado na furaha ambapo alipost picha akiwa yeye na mpenzi wake Cherry Seaborn na aliandika "Climbing mountains in peru".

Baadhi ya mashabiki wameonesha kusikitishwa sana na jambo hilo kama baadhi ya Tweets zinavyoonekana toka kwa mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki huyo.



                                 

Pages