Drake na Upande wake Wa Pili, Kutengeneza Mpunga - teknomovies
Drake na  Upande wake Wa Pili, Kutengeneza Mpunga

Drake na Upande wake Wa Pili, Kutengeneza Mpunga

Share This
DrakeMsanii mkali Tokea pande za Canada Akifanyia kazi zake, Marekani Jana amepost picha katika mtandao wake wa Instagram akionesha Hundi ya Hela ambapo inaonesha Bado anatengeneza Mkwanja kupitia ishu zingine.

Katika Picha hiyo Drake alionesha Hundi ambayo inaonesha mkwanja kauvuta toka Series Ya Degrassi ambayo drake kawahi kuigiza ndani.
A post shared by champagnepapi (@champagnepapi) on


katika Series Hiyo Drizzy alicheza kama Jimmy Brooks kuanzia mwaka 2001 mpaka 2005 alipoamua kuachana na Series Hiyo na kuwekeza nguvu katika mziki wake.

Mwaka 2016, Billboard walimtaja Drake kushika namba 4 katika chati ya wasanii 50 walioingiza mkwanja zaidi akiingiza hela sana kupitia mauzo ya kazi zake pia na Matamasha yake.

Lakini bado Drizzy ajaacha kabisa kuigiza, kwani mwaka 2015 alirudi tena katika Series Hiyo kwa Vipande kadhaa ambapo katika moja ya Interview Drake alisema Kua hakuna aliyemwambia kuhusu mambo ya Filamu ni yeye aliyeamua kucheza, Japo kwa Sasa malengo yake makubwa yapo katika muziki lakini bado anapenda kufanya Filamu sababu ndiko sehemu alikoanzia.

Mwezi April Taarifa zilitolewa kua Jamaa ataonekana pia kwenye Series toka uingereza itayokwenda kwa jina La "Top Boy"

Pages