Neno "Ninja" Asili yake inatokana na mchezo wa mapigano ya kiasili ya Japan yanayohusisha silaha mbalimbali kama pinde,mishale ya mianzi yenye sumu ya kupuliza, vyuma virushwavyo vyenye sumu, mapanga au majambia, nguvu za Giza au uchawi, mapigano hayo huitwa "Ninjitsu" na yalikuwa yakifanyika kwenye miaka ya 900-1200 AD huko Japan.
Mara nyingi “Ninja” hao walikuwa wakitumika kwa mauaji ya watu waliokuwa wakitakiwa wafe, aidha kwa kulipizana visasi au wadaiwa, au ugomvi wa koo na familia juu ya Mali, mashamba nk. Na Mara nyingi kiasilia walikuwa wakifanya mauaji yao USIKU WA MANANE TU NA SIYO MCHANA. . .
Wanavamia na kufanya uharibifu na kutoweka bila kujulikana. Walikuwa na uwezo wa kupanda ukuta kama paka, miti kwa speed ya ajabu, kutembea juu ya mapaa ya nyumba, kutoweka ghafla(invisibility), na mengineyo ya kishirikina/ajabu.
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.