Marvel Wanakuja Na Nondo Nyingine Hii Hapa. - teknomovies
Marvel Wanakuja Na Nondo Nyingine Hii Hapa.

Marvel Wanakuja Na Nondo Nyingine Hii Hapa.

Share This

Kuna ndugu zangu wanaopenda michongo kama hii na wengine hawapendi hata kidogo, mfano mzuri ni Kaka yangu ambaye Movie yoyote yenye Usayansi ndani yake kwake Hata kidogo Hazipendi Vibaya mno. 

Lakini Tambua mojawapo ya movies ambazo zinatumia gharama kubwa sana katika maandalizi na pia huwa na mauzo makubwa Kamwe huwezi kuacha kuzitaja, movies zenye usayansi wa kufikirika ndani yake.

InHumans ni movie mpya inayokuja ambayo itaoneshwa katika mfumo wa IMAX Kwa Takribani week 1 Kuanzia September 01 na baadae itaachiwa Series yake ambayo itakua na Episodes  8 kuanzia September 29.

Ikiwa imeandaliwa na makampuni mawili, Marvel Studios na Abc Studios pia, ambapo kwa upande wa Series Itaoneshwa na Chaneli ya ABC.

Watu wengi wanaisubiria kwa hamu, kwanza kutokana na kuja katika mifumo miwili yani, Movie na Series, hivyo Ubora wa movie ndio utaofanya Series ipendwe zaidi na wapenda movies duniani.

FrankDaxx Media itaendelea kukujulisha kila kinachoendelea katika ulimwengu wa movies, Cha msingi usiache kutufuatilia kupitia mitandao ya kijamii ,Fb, Twitter na Instagram @FrankDaxx.

Pages