YUKO WAPI TOBEY MAGUIRE (SPIDERMAN WA KWANZA) - teknomovies
YUKO WAPI TOBEY MAGUIRE (SPIDERMAN WA KWANZA)

YUKO WAPI TOBEY MAGUIRE (SPIDERMAN WA KWANZA)

Share This

Mwaka 2002 Filamu Bora Ya Spider Man Iliachiwa Ambapo Ilifanya Vyema Sana Katika Box Office Ikiuza $821.7M..Na Ndo Filamu Hii Ambayo Ilitupa Jina Jipya Katika Ulimwengu Wa Filamu La Tobey Magure.

Tobey Alipata Sifa Kem Kem Kupitia Filamu Hiyo, Na Haikushangazwa Kumuona Tena Katika Spider Man 2 Na Pia Ya 3 Lakini Ghafla Watu Wengi Wakashangaa Kwa Kuzimwa Kwa Mtu Huyu Ambaye Unaweza Sema Kafariki Hivi.

Tobey Maguire Ni Nani Haswa?

Alizaliwa June 27 Mwaka 1973 Toka Kwa Mwanamama Wendy Maguire Ambaye Alikua Ni Producer Pia Alikua Ni Screen Writer Na Baba Yake Alikua Ni Construction Worker.
Akiwa Na Miaka Miwili Tu Wazazi Wake Walitarakiana Hivyo Kupelekea Kuishi Kwa Kuhama Hama Sana, Yani Muda Huu Kwa Mama, Mara Kwa Baba Mara Kwa Ndugu Na Kufanya Utoto Wake Kukua Kwa Shida Kidogo.

Akiwa Shule Alikua Anapenda Kuja Kua Mpishi, Ila Mama Yake Hakupenda Hicho Ambapo Ilibidi Afanye Jambo Kwakumuhonga Mtoto Wake Dollar $100 Ili Shuleni Achukue Masomo Ya Filamu Na Kweli Alifanikiwa Mtoto Wake Akaanza Kusomea Mambo Hayo.
Kipindi Cha Shule Tobey Alikua Ni Mtu Wa Stress Sana Na Alikua Anashindwa Kumanage Kua Na Marafiki Mara Zote Alikua Akikosana Na Marafiki Na Pia Chanzo Kikuu Ilikua Ni Kuhamishwa Hamishwa Shule.

Badae Alikuja Kufukuzwa Shule na akaamua Rasmi Kuingia Katika Maswala Ya Filamu Huku Kielimu Akapiga GED Hii Kwa Marekani Ni Mfano Kama QT Kwa Bongo.


Muda Wa Mwangaza Ulianza Hapa.

Mwaka 1989,Ndo Nuru Yake Ilianza Kuonekana Baada Ya Kucheza Katika Movie Ya The Wizard As A Supporting Role Ambayo Ilianza Kumtambulisha Tambulisha.

Kuanzia Mwaka 1990's Alianza Kucheza Katika Baadhi Ya Tv Shows Mbalimbali Na Hadi Kufanya Kazi Na Baadhi Ya Mastar Wa Kipindi Hicho Kama Chuck Norris Na Leaornado Di'caprio.
Baadae Alipata Lead Role Katika Drama Kutoka Fox Tv Lakini Baada Ya Mchongo Huo Kurushwa Kwa Week Tano Ukasitishwa.

Kwa Kipindi Hicho Alikua Kashaanza Kua Star Haswa Ambapo Ilipelekea Kuanza Kufanya Starehe Sana Hasa Utumiaji Wa Pombe Ambao Ulianza Kuathiri Kipaji Chake.. Ila Ni Kama Alijistukia Yeye Mwenyewee Alijipeleka Sober Ili Kuacha Tabia Hiyo Na Kweli Alifanikiwa.

Mwaka 1997 Alipata Deal Katika Filamu Ya Ice Storm... Ambapo Zilifuata Filamu Zingine Kama Pleasantville, The Cider House Rules, Wonder Boys Na Hapo Ikawa Imempa Nafasi Zaidi Kubwa Ya Kujulikana.

Mwaka 2002 Ndo Umaarufu Ulikua Zaidi Kwa Haraka Kupitia Filamu Ya SpiderMan.. Na Badae Akapita Katika Msimu Wa Pili Na Wa Tatu Ambapo Hapo Ndo Ikawa Mwisho Kwake.


Nini Kilifuata Baada Ya Hapo?!

Wakati Mkakati Wa Kuja Na Spider Man 4..Ghafla Project Nzima Ilisitishwa Kwanza Ilikua Ni Kutokufikiana Maelewano Kati Ya Director Ambae Ni Sami Raimi Aliyeongoza Vyema Sana Part 1 Mpaka 3...pamoja Na Waigizaji Ambao Ni Tobey, Kristen Durnst Pamoja Na Jeremy Franco Na Uongozi Wa Sony.

Kusitishwa Huko Kuliwafanya Sony Kuianzisha Upya Kabisa SpiderMan Na Safari Hiyo Wakitaka Kijana Mdogo Mdogo Sana.. Tofauti Na Tobey Ambaye Alikua Kaanza Kua Kijana Kijana.
Hapo Ndo Mchongo Ulidondoka Kwa Andrew Garfield Na Ndipo The Amazing Spiderman 1 and 2 Zikafanyika Lakini Toka Spiderman 3 Tumuone Tobey Ndo Imekua Mara Ya Mwisho Kuonekana Machoni Pa Watu.

Mwaka 2007 Alionekana Tena katika Series Ya World Series Of Poker lakini Hakudumu Saana.
Baadae Alionekana Katika Roles Ya Baadhi Ya Movies Tena Pembeni Ya Wakali Kama Leonardo DiCaprio Movie Ikienda Kwa Jina La The Great Gatsby.

Alionekana Pia Katika War Drama Ya BROTHERS ambayo Ilimrudisha Kimtindo Masikioni Mwa Watu Baada Ya Kutajwa Katika Baadhi Ya Kipengele Katika Tuzo Za Golden Globe Award Ambapo Hadi Yeye Mwenyewe Tu Alishangaa Maana Hakutegemea Kabisa Hivyo Kutajwa Kwake Tu Katika Tuzo Hizo.. Ilikua ushindi Tosha.


Kwa Sasa Anafanya Nini?!

Yupo kimya Sana Kwa Sasa Na Yote Ni Kutokana Kuhamia Sana Katika Sekta Ya Uprodyuza Ambapo Alianza Toka Mwaka 2002,Ambapo Kazi Hiyo anaifanya Katika Kampuni Yake Mwenyewe Ya Mambo Ya Movies Na Ndicho Kilichomfanya Zaidi Asionekane Lakini Ni Ukweli Usiopingika Kua SpiderMan Itabaki Kua Filamu Iliyompa Umaarufu Zaidi Na Hiyo Hiyo Tena Kumshusha Tena Chini Lakini Pia Ni Ukweli Usiopingika Kua Jamaa Atabaki Kua Ndo SpiderMan Bora Kuzidi Wengine Wanaokuja.


Usisahau KutuFollow @teknomovies Instagram and Twitter.

No comments:

Post a Comment

Pages