NICOLAS COPERNICUS,ALIPINGWA ALIPOSEMA DUNIA INAZUNGUKA JUA#UCHAMBUZI - teknomovies
 NICOLAS COPERNICUS,ALIPINGWA ALIPOSEMA DUNIA INAZUNGUKA JUA#UCHAMBUZI

NICOLAS COPERNICUS,ALIPINGWA ALIPOSEMA DUNIA INAZUNGUKA JUA#UCHAMBUZI

Share This
Mwana-Astronomia Nicolaus Copernicus aliyezaliwa tarehe 19 mwezi Februari mwaka 1473, alikuwa ni mwanasayansi wa Kwanza ku-
suggest kwamba Dunia na Sayari nyingine zinazunguka Jua, badala ya mtazamo uliokuwepo mwanzo, kwamba: Dunia ndio iliyokuwa center, na kila kitu kiliizunguka…

Ili kumwelewa zaidi Nicolaus, ni vizuri tukielewe kipindi alichozaliwa…
Copernicus alizaliwa na hatimaye kufa katika sehemu iitwayo “Royal Prussia ” iliyoko nchini Poland.

Lakini, nahisi cha msingi zaidi kufahamu, ni kwamba: Copernicus alizaliwa katika kipindi cha Historia Ulaya kinachoitwa “Renaissance

RENAISSANCE:

“Renaissance” au “Enlightenment Age” (Zama za Mwamko) ni kipindi cha Ki-Historia cha Ulaya kilichoanza karne ya 14 mpaka ya 17. Kilianzia Italia, na hatimaye kusambaa sehemu nyingine pia Ulaya.

Ni kipindi ambacho kwa kweli kilileta mwamko mkubwa sana wa maendeleo katika Sayansi, Falsafa, Siasa, Teknolojia na Sanaa pia.

Neno “Renaissance ” linatokana na neno la Kifaransa lenye maana ya “Kuzaliwa Upya”. Sababu zilizopelekea kipindi hiki kuitwa hivyo ni kwamba, wakati huo, watu walianza kuwa na shauku kubwa ya Kujifunza, Kutengeneza na Kugundua. Na, ni katika kipindi hiki waliishi watu kama Leonardo da Vinci, Galileo Galilei, Johannes Kepler, na wagunduzi kama Christopher Columbus.
(waweza fanya research zaidi juu ya kipindi hiki cha Historia, kwani ni cha kusisimua sana)

Turudi kwa Copernicus:

Copernicus alisoma katika Chuo cka Krakow nchini Poland, na alisomea Hisabati pamoja na Astronomia. Alikuwa mzuri katika: “Geometry”, “Arithmetic”, “Cosmograghy ”, pamoja na “Theoretical & Computational Astronomy ”.

Copernicus pia alikuwa influenced na kazi za MwanaFalsafa Aristotle kupitia vitabu vyake kama: “De coelo ” na “Metaphysics”

Katika kipindi cha Copernicus, wengi waliamini kwamba, Dunia ndio ilikuwa katikati ya Ulimwengu (Universe), na kila kitu, yaani sayari zote pamoja na Nyota viliizunguka Dunia.

Mfumo huo wa Dunia ikiwa center unaitwa “Geocentric Model ” au “Ptolemaic System ”. Mfumo huu wa Ulimwengu ulikuwa umeshika hatamu kwa muda mrefu, na wanaFalsafa maarufu kama Aristotle na wanaAstronomia kama Ptolemy, wote pia walidhani hivi ndivyo Ulimwengu ulivyokuwa.

Kimsingi, siwezi kuwalaumu, au kuwaona wajinga kwa kuamini hvyo, kwani hawakuwa na vifaa au Teknolojia tulizonazo leo. Ufahamu wao wa Ulimwengu ulitokana na vile walivyoweza kuvi- observe (kuviona) kwa macho yao.

Observation zilizoi-support idea hiyo ya “Geocentrism” zilikuwa mbili:

Ya Kwanza ni kwamba: Jua, pamoja na Sayari zili- appear kama vile zinaizunguka Dunia kila siku. Na pia: Kila nyota ilikuwa kwenye “stellar ” au “celestial”; mfumo wa Duara, na Dunia ndio ilikuwa katikati. Nyota zilizokuwa karibu na Equator zilionekana kupanda na Kushuka Umbali mrefu, lakini kila nyota ilizunguka kufikia pale inapopanda kila siku.

Observation ya pili ni kwamba: Dunia haionekani kuzunguka, kwa mtu ambaye yupo ndani ya Dunia, kwahiyo hali hii ikawafanya kudhani au kufikiri kwamba Dunia ipo “stationary ”, yaani Imesimama.

Mfumo huo pia ulitumika kubashiri misimu mbalimbali katika mwaka, pamoja na majira.
Tatizo kubwa la Ki-Hisabati katika mfumo huo wa Ki-Geocentric ni kwamba: Kuna kipindi Sayari zilionekana kusafiri kinyume ukizitazama angani. Wana-Astronomia waliita hali hii “Retrogade motion ”.

Ili ku-deal na tatizo hilo, mwana-Astronomia na mwana-Hisabati Ptolemy aliongeza miduara katika miduara iliyokuwepo katika mfumo huo, na kuiita “epicycles ”. Kwa kuongeza miduara, iliifanya mfumo huo kuwa complicated, kiasi cha kufikia Sayari nyingine kuwa na miduara hadi saba.

Mwaka 1514. Copernicus alisambaza kitabu chake alichokiandika kwa mkono. Kitabu hiki kiliueleza mfumo wake mpya, ulio-suggest kwamba: Center ya Ulimwengu haikuwa Dunia, bali ilikuwa ni Jua.
Ali-suggest pia kwamba Dunia inapojizungusha kwenye axis yake (Rotation), husababisha machweo na Kuzama kwa Jua. Aliendelea pia kwamba mwonekano wa nyota pamoja na majira Duniani hutokana na Dunia kulizunguka Jua.

Mwishoni, pia akamaliza kwa ku-suggest kwamba ile “retrogade motion” inayoonekana katika mfumo wa “Geocentric” inatokana na Dunia inapotembea katika Anga (Space )
Kitabu chake kilichoitwa “De Revolutionbus Orbium Coelestium”, tafsiri: “On the Revolutions of the Heavenly Spheres” hakikuchapishwa mpaka alipokuwa na miaka 70 (karibu na kifo chake). Katika Kitabu hichi, Copernicus aliuelezea mfumo wake, wa Jua kama Center badala ya Dunia, na akafafanua kuhusu mfumo wa Jua (Solar System ) pamoja na njia (paths ) za Sayari.

Pamoja na kwamba mfumo huu wa Copernicus ulichangia kwa asilimia kubwa sana namna tunavyouona Ulimwengu hivi leo, bado ulikuwa na mapungufu kadhaa. Kwa mfano: Copernicus bado aliamini katika idea ya muda mrefu kwamba Sayari zilizungua katika “perfect circle ”, nadharia ambayo ilikuja kukanushwa mwaka 1600 na Johannes Kepler, aliye-suggest kwamba Sayari hazikunguka in “perfect circles ” lakini zilizunguka in “ellipses

Copernicus alifariki tarehe 24, Mei 1543, miezi miwili tu baada ya kitabu chake kuchapishwa. Lakini, hata baada ya kuchapishwa, bado watu hawakuuchukulia maanani mfumo huu wa Copernicus. Ilichukua takribani miaka 100, mpaka mwaka 1632, pale Galileo Galilei alipoonyesha na kueleza zaidi, kwanini Dunia huzunguka Jua.

Mpaka leo, Nicolaus Copernicus anaheshimika kwa mchango wake mkubwa sana katika uelewa wetu tulionao hivi leo kuhusu Ulimwengu. Na, ndio maana tunaiita model ya Solar System kama “Heliocentric ” au “Copernican Model
Mimi, personally Nicolaus Copernicus ni mmoja kati ya mashujaa wangu (one of My Heroes)!

No comments:

Post a Comment

Pages