USIYOYAFAHAMU KUTOKA KWA BUSHMAN (THE GODS MUST BE CRAZY) - teknomovies
USIYOYAFAHAMU KUTOKA KWA BUSHMAN (THE GODS MUST BE CRAZY)

USIYOYAFAHAMU KUTOKA KWA BUSHMAN (THE GODS MUST BE CRAZY)

Share This
Nǃxau ǂToma (Kwa ufupi inatamkwa Nǃxau) mzaliwa wa Namibia, alizaliwa tareh 16 December 1944 na kufariki tareh 5 July 2003. N!xau alikuwa actor aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia movie aliyocheza mwaka 1980 ya "The Gods Must Be Crazy" umaarufu wake haukuja tu kwa sababu ameigiza kwenye movie bali namna alivyoigiza ndio kitu kilichompa umaarufu.


Nimekuwekea hapa vitu unavyopaswa kujua kutoka kwa Bush Man huyu.

1. Mpaka anafariki N!xau alikuwa hajui umri wake sahihi na kabla ya kuigiza movie ya The Gods Must be Crazy alikuwa hajui kama duniani kuna maisha ya kifahari (luxury life) ya kuendesha gari na kutumia simu.







2. Kwa mujibu wa gazeti la Namibia ni kwamba N!xau alikuwa hawezi kuhesabu zaidi ya 20. Yaani akipewa kazi ya kuhesabu basi anaanza 1 hadi 20 hawezi kuendelea mbele.

3. Director wa movie Jamie Uys alitumia miezi mitatu nchini Afrika Kusini kutafuta muhusika mkuu wa movie mpaka alipokuja kukutana na N!xau Botswana na hapo N!xau kwa mara ya kwanza akawa amekutana mtu mweupe (mzungu) na akashawishiwa hadi akakubali kwenda New York kwa ajili ya makubaliano ya kutengeneza movie.







4. Director alimlipa Bushman $300 kwa siku 10 alizofanya kazi, baadae akagundua kuwa alifanya kosa kwa sababu mtu aliyempa hela hajui thamani yake wala matumizi yake kwa hiyo malipo ya pili akampa ng'ombe 12 kufika nao kijijini ng'ombe 8 wakaliwa na simba, alichokifanya hakumpa tena badala yake akafungua account akamuwekea $20,000.

5. N!xau alibadili dini mwaka 2000 na kuwa mkristo wa dhehebu la Sabato.

6. N!xau ameigiza filamu kadhaa ikiwemo The Gods Must Be Crazy II, Crazy Safari , Crazy Hong Kong na The Gods Must Be Funny in China. Baada ya kumaliza kuigiza filamu alirejea nyumbani kwake  Namibia na akawa mkulima wa Mahindi, Maboga na Maharage pamoja na kufuga ng'ombe ila ng'ombe walikuwa hawazidi 20 mana yeye mwisho wake kuhesabu ni 20.

Pages