Mayweather Sr ashtakiwa kwa kumshambulia mwanamke - teknomovies
Mayweather Sr ashtakiwa kwa kumshambulia mwanamke

Mayweather Sr ashtakiwa kwa kumshambulia mwanamke

Share This
Floyd Mayweather Sr ambae ni baba mzazi wa Mayweather Jr ameshtakiwa kwa kosa la kufanya shambulio kwa mwanamke katika pambano kati ya Canelo Alvarez vs Gennady Golovkin huko Las Vegas mapema mwezi September.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa tukio hilo limetokea tarehe 17 September baada ya kumalizika kwa pambano ambapo Mayweather alitumia nguvu kumtoa ndani ya gari mwananmke ambae aligoma kutoka. Mayweather alimuamuru mwanamke huyo kutoka ndani ya gari lakini alipogoma alimvuta miguu na kumtoa nje na pia akampiga ngumi ya mguu.

Baada ya tukio hilo mwanamke alipata majeraha ambayo alienda kutibiwa Hospitalini

Mayweather Sr alikuwa bondia kati ya miaka 1970 hadi 1990

No comments:

Post a Comment

Pages