3 Idiots Review - teknomovies
3 Idiots Review

3 Idiots Review

Share This
Ndani unamkuta mtu mzima Aamir Khan, mrembo wetu Kareena Kapor, Sharman Joshi na Wengineo wengi.

Iliachiwa mwaka 2009, ambapo kwa kipindi hicho iliweza kuweka baadhi ya rekodi kama, Filamu iliyoingiza pesa nyingi sana kwa siku moja tu ilivyoachiwa na pia iliweka rekodi ya kuingiza hela nyingi kupitia mfumo wa kimtandao wa kimauzo.

Hii ni Mojawapo ya Filamu chache kutoka India ambazo kwa nchi nyingine iliweza kua adapted kama nchi ya Mexico waliifanya kivyao nao pia.. Stori na matukio mengi yakiwa sawa tu.

Utapotazama hii filamu, Itakupa elimu ya Urafiki mzuri ni upi...Kama jina lilivyo " 3 Idiots " kwa Tafsiri isiyo rasmi "Wajinga Watatu" Inahusu Marafiki Watatu waliokutana Chuo Cha Engineering, Lakini Kila mmoja nyuma alikua na yake mambo yalimfanya Kila mmoja kukutana hapo katika chuo Cha Engineering.

Tuanze na Farhan, toka muda alikua ana ndoto ya kua bonge la mpiga picha, lakini aliamua kusoma Engineering sababu ya kumuogopa Baba yake.

Raju yeye, Aliamua kusoma Kozi hiyo kwaajili Ya kuipa sapoti Familia yake lakini alikua Anapata matokeo mabovu kutokana na kukosa "Kujiamini"

Ukija kwa huyu Chizi Rancho..alikua Bonge la Genius, Yeye muda wote alikua anafanya fanya Ujinga tuu.. Lakini darasani alikua nondo balaa... Kuna kauli moja alikua anapenda kuwaambia wenzake.. Maana walikua wanasoma saana ili kupata maksi nzuri ili waje kuajiriwa na Kampuni nzuri.

Yeye alikua anawaambia, "Fanya Kila kitu kwa ubora, utaona mafanikio yanavyokuja, Usiwaze mafanikio bali waza Jambo unalolifanya, Liwe bora.. Sababu siku zote mafanikio Huja Katika sehemu bora" wenzake walikua Hataa hawamuelewi.

Ndani utafurahi kuna, Mwalimu mmoja alikua na Beef na kundi lao... Walikua wanamuita "Virus" Limwalimu hilo bhana, kwanza lilikua linaamini mtoto yoyote ya kiume ni lazima asome mambo ya Engineering na kwa mtoto wa kike, lazima asome mambo ya medical.

Ilikua inasemekana, mtoto wake wa kiume alijiua sababu ya Kulazimishwa kusoma Engineering, wakati yeye alipenda kuja kua Mwandishi.

Mtoto wake wa kike ndo Kareena kapor.. Yeye alifuata Baba Anachotaka... Alikua Daktari na ndiye alikua Rancho Girlfriend wake.... Sasa Rancho alikua ana mambo mengi sana, afu mengi yalikua kama ya Kitoto toto sana, mpaka akawa anawapoteza wenzake.. Kuna Tukio moja Walifanya, Walizamia kwenye Sherehe ya Harusi ya Mtoto wa Ticha Wao Virus....

Huko walijipakulia Ma misosi, alafu ndiko sehemu alikokutana na mtoto Kareena Kapor, Alimtia mtoto sumu za ukweli...Demu alikua na mshikaji wake ambaye walikua wanategemea Kuja nao kufunga ndoa muda si mrefu, lakini yule Jamaa alikua anajali sana Pesa kuliko vitu vingine, huku kila kitu kwake akifanya measures kwa pesa, Mfano Ukiaribu Nguo Yake utakuta lazima atasema "Pumbafuuu Umearibu nguo yangu nimenunua laki mbili"

Sasa Rancho alimwambia mtoto kwamba Ukiolewa na huyo jamaa, Utapata shida sana, sababu yeye anakuona kama Bidhaa kwake, kwanza angalia amekununulia Saa hiyo ya Bei, Mfano ukipoteza Hiyo Saa anakushusha Thamani... Mfano ngoja Nikuoneshe.. Akamvua saa, Alafu akamwita mchumba wa Demu, Akamwambia Baby wako kapoteza Saa... Jamaa Lilipiga Kelele Hilo.. Pumbafuu yani Nimenunua Saa Bei kali alafu unapoteza Leoo.. Shenzi naomba Uipate Hiyo Saa... Demu Akajua Hapa Kweli sina Bwana.

Aisee Kuna Matukio mengi, Ushawahi soma wale kazi Yao Ni kupenda Sifa Na Hawana bahati.
Kuna Jamaa alikua anaitwa Silencer... Yeye alikua anashindana na Rancho, na Kila sehemu alikua anapigwa chini, Japo lilikua linajitahidi kukesha kweli Kweli, Ila Ujinga wake yeye alikua anafurahi kuwapoteza wengine, Ili yeye afaulu.

Bonyeza Hapa Kuipata Filamu Hii.

Pages