Mallette anasimulia kua kipindi cha utoto wake kwa asilimia
kubwa kilitawaliwa na manyanyaso ya kingono na matukio ya vurugu vurugu,na hapo
alikua bado mdogo alipoanza kukumbana na hayo mambo,akiwa na miaka 3 tu.
Tunaposema alikua
akikumbana na manyanyaso ya kingono,maana yake ni kua alikua akipigishwa kwichi
kwichi kuanzia akiwa na umri mdogo na watu aliowataja katika kitabu chake kua
alikua ni muangalizi wake wa kiume wengi mnawaitaga babysitter,sasa kwake yeye
alikua ni wa kiume ambaye ndiye alikua akimpa mambo ya kikubwa. Pia anamtaja
mtu mwingine kua ni rafiki wa babu yake pia naye alikua akimpa huo mchezo na wa mwisho anaowataja walikua ni watoto wa
nyumba za jirani nao walikua wanaparamia.
![]() |
Justin akiwa na Mama kipindi akiwa mdogo |
Anaandika “ nilikua nikinyanyaswa
mara kwa mara kiasi kwamba hali hiyo kwangu nilianza kuizoea na kuiona ndo kawaida yangu. Kiukweli ni ndoa ya
ajabu,unajua jambo flani ni hatari lakini muda huo huo unaona ndo kawaida kwako
na ndiyo ilivyo sehemu nyingine”
Alipofikisha miaka 14 bado manyanyaso ya kingono alikua
akiyapata ila alipofikisha miaka 15 kuna
tukio baya lilimtokea,ila kutokana na maisha aliyopitia nazani kwake ilikua
kawaida. Tukio lenyewe Lilikua ni kubakwa.
UJANA WAKE.
Tangu akiwa mdogo alikua
akipenda kuigiza na pia kuimba hiyo ilionekana zaidi kwani alishiriki
katika matamasha na baadhi ya tamthiliya kama POMPER ROOM na pia BIG TOP TALENT hizo zilikua baadhi ya michezo ya television
ya watoto iliyokua ikiwashindanisha watoto
kula.
Alipofikisha miaka
kumi alishiriki katika mchezo wa kuigiza
stejini ukifahamika Stratford Shakespeare ,mchezo ambao ulikua
ukiwaleta watalii wengi katika mji wao. Akiwa shule alikua akishiriki katika
michezo mingi ya kuigiza na pia kuimba,pia hata kucheza michezo ambayo ilimpa
mataji mengi sana ambapo alipata nafasi ya kua managed na manager ambaye alikua anatokea mji wa torronto lakini
kabla ya mambo hayajakamilishwa ambapo alitakiwa yeye kua anakwenda kila week
ila wazazi wake walishindwa kufanya Hivyo na kumuacha mallette akikasirika sana
kutokana na hilo tukio.
Miaka 14 hapo ndo mambo yalizidi kuharibika zaidi kwani ndo
umri ambao alianza kutumia madawa ya kuleya hususani pombe,bangi pamoja na
madawa flani yanayofahamika kama LSD(Lysergic acid diethylamide) . kutokana na madawa hayo
alisimamishwa shule hiyo ni baada ya kusababisha moto akiwa bafuni huko huko
shuleni hayo mabangi yake.
Akiwa na miaka 15 ndipo alipoanzisha mahusiano yake na baba
wa mzazi wa justin bieber, akifahamika kwa jina la Jeremy bieber ambapo
mahusiano yao yalidumu kwa miaka 4.
Miaka 16 alipofikisha aliondoka home na kuanza kujitegemea
lakini kazi alizokua akifanya sasa,udokozi wa hapa na pale pamoja na uuzaji wa
dawa za kulevya. Kwa kipindi hicho alianza kufanya matukio ya ajabu zaidi ila
zaidi alikumbwa na upweke hiyo ni baada ya
kutengwa hali iliyompelekea
kutaka kujiua mara kadhaa kama tukio moja ambapo alijirusha toka kwenye gari
likiwa linatembea hapo akiwa na miaka 17,
Kutokana na tukio hilo,alipelekwa katika hospitali za
wagonjwa wenye matatizo ya akili na akiwa huko ndipo mabadiliko yalianza kutokea
ambapo aliamua kuokoka na kua mkristo safi.
Baada ya kuachiwa toka hospitali aliamua kuanza kurudisha
mahusiano mazuri yaliyopotea akianza na wazazi wake na baadae walirudiana na
Jeremy bieber ambapo miezi 6 baadae
alipata mimba ambapo alijifungua march 1 mwaka 1994 ndo akatupa kipaji kinachopendwa sana na watu
ulimwengu huu. Baada ya kujifungua yeye
pamoja na Jeremy waliendelea kua na mahusiano lakini baadae waliachana lakini
bado walikua wakishirikiana katika matunzo ya mtoto.
MUSIC
Justin bieber tangu akiwa na miaka 2 alionesha kua anapenda
kuimba na mama yake ndiye alimpa sapoti tosha mfano kama kumpeleka katika
baadhi ya mashindano ya kuimba. Shindano linalokumbukwa sana na watu wengi ni
shindano lililokua likifamika kama “Stratford
Star” ambapo aliimba wimbo wa Neyo
so sick ambapo alimaliza nafasi ya pili katika shindano hilo.
Mama alipost video
hiyo youtube kwaajili ya marafiki zake na familia zingine kuona na aliendelea
kufanya hivyo jambo lililopelekea umaarufu kwa mtoto wake kukua zaidi
mtandaoni.
UANDISHI
September mwaka 2012 aliachia
kitabu kikielezea maisha yake alikipa jina la Nowhere up ambapo ndani alizungumzia matatizo mbalimbali aliyopitia
pamoja na mabadiliko yake toka kuchukiwa na kua mama pekee akimlea mtoto wake
justin.
Kwa week moja kitabu chake kilishika nafasi ya 17 kutoka new York best seller list, kitabu
chake kwa dunia nzima kimesomwa sana na
pia kupewa thamani nzuri na kimekua kitabu ambacho kimekua kikifanyiwa review
mara kwa mara katika media tofauti tofauti.
No comments:
Post a Comment