WATALII 2 WAKAMATWA NCHINI DUBAI BAADA YA KUPEANA UJAUZITO. - teknomovies
WATALII 2 WAKAMATWA NCHINI DUBAI BAADA YA KUPEANA UJAUZITO.

WATALII 2 WAKAMATWA NCHINI DUBAI BAADA YA KUPEANA UJAUZITO.

Share This

Watalii 2 wamekamatwa nchini Dubai baada ya kugundulika wamefanya mapenzi hali ya kuwa hawajaoana hii ni baada ya daktari kutoa taarifa polisi baada ya kumpima msichana na kugundua ni mjamzito.

Mwanamke huyo kutoka Ukraine na mpenzi wake kutoka Afrika kusini walikamatwa huko Dubai baada ya kufanya mapenzi ilhali si wanandoa .






Kwa mujibu wa mtandao wa Netwek 24, mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Iryna Nohai (27) na mpenzi wake Emlyn Culverwell (29) walikuwa na time nzuri huko dubai wakibarizi maeneo ya beach ndipo Iryna akaanza kupata maumivu kwenye tumbo, akapelekwa hospitali na daktari akathibitisha kuwa ni mjamzito.







Wakati Iryna anaendelea kupatiwa matibabu mmoja wa madaktari akatoa taarifa polisi juu ya ujauzito wa msichana huyo ilhali si wanandoa ni wapenzi tu.

Muda mchache baadae polisi walifika na kuwakamata wote wawili kwa kufanya mapenzi wakiwa si wanandoa kitu ambacho ni kinyume cha sheria katika falme za kiarabu (UAE).

Mama wa mtoto mwenye ujauzito amesema wanataka kumpima ili wajue no ujauzito wa miezi mingapi.




Kwa sasa balozi za Ukraine nchini Dubai zinapitia report ili watoe mrejesho ikiwa waoane au wafukuzwe nchini humo.


No comments:

Post a Comment

Pages