Mwaka 2017, Tecno walifanikiwa kuachia matoleo matatu makuu, ambayo ni Phantom,Camon na sasa wamekuja pia na Spark.
Katika uchambuzi huu,tumeangalia Toleo la Spark ambalo limekuja mwishoni mwa mwaka 2017. Katika Toleo hilo mpaka sasa wameachia simu mbili ambazo ni Spark K7 na Pia Spark Plus K9,Tunaangalia utofauti wake ili kwa mtu ambae anataka kwenda kununua ajue sifa zake poa.
Display
Hapa ni katika Kioo, ambapo huwa tunaangali namna inavyoonesha. Spark K7 kioo chake ni HD, ambapo kina ukubwa wa Inch 5.5 na ubora wa muonekano ni umewekwa kwa 720 kwa 1280 lakini kwa upande wa Spark Plus K9 kioo chake ni kikubwa kidogo kikiwa na ukubwa wa Inch 6.0 lakini kuonesha muonekano wa picha ni sawa na K7 ikiwa nayo na 720 kwa 1280.
SOMA PIA: THE PUNISHER, MZIGO MZIMA KICHAPO MWANZO MWISHO
Katika Eneo hili simu hizi hazina utofauti mkubwa sana sababu kila simu ina uwezo wa kuonesha picha yenye ubora zaidi, na kukupa burudani zaidi pale unapotazama kitu fulani au unapotazama picha.
Memory na Os
Katika sehemu hii, Upande wa Ram Spark K7 ina ukubwa wa GB 1 wakati Spark Plus K9 ina ukubwa wa Gb2.
Upande wa Memory ya ndani zote kwa pamoja zina Ukubwa wa GB 16 wakati unaweza kuongeza mpaka memory yenye ukubwa wa GB32.
Na kwa upande wa Toleo Endeshaji zote kwa Pamoja zina toleo la Android 7.0 Nougat na pia Hios 2.0 ambayo ina uwezo mkuu wa kumfanya mtu kutumia simu katika mambo mengi.
Procesa
Katika upande wa Procesa K7 inatumia Prosesa ya Octacore 1.3 GhZ pia na K9 inatumia Prosesa ya Octacore ya 1.5 Ghz.
SOMA PIA: SPIDERMAN KUJA NA ANIMATION
Ukubwa wa prosesa ni muhimu sana katika kukupa spidi nzuri ya Simu kipindi unapotumia katika kuperuzi mambo mbalimbali.
Camera
Upande wa Camera zote mbili, Katika kamera za nyuma zina ukubwa wa 13MP na kwa upande wa Camera za mbele zina ukubwa wa 5MP Huku zikiwa na LED Flash,Face detection na mambo mengine.
LED Flash zote ni moja hivyo itasaidia katika kuboost pale unapotaka kupiga picha katika mazingira mabaya.
Battery
Upande wa Battery hapa upande wa K9 lina uwezo wa 3400 mAh na K7 ina uwezo wa 3000 mAh. Zote kwa upande wa chaji zitakupa uwezo mkubwa wa kutumia Simu yako kwa masaa mengi bila kuweka chaji.
Kama utajaza Full, utaweza kutumia kwa zaidi ya masaa 13 Bila kuweka chaji tena.
SOMA PIA>> WAHINDI KUJA NA FILAMU YA RAMBO KIVYAO
Baadhi ya Mambo mengine pia ni kama uwezo wa kuweka Alama ya kidole kama Alama ya kufungulia Simu pamoja na Simu zote uzito zikiwa zimetofautiana kidogo lakini katika Ubora zote Simu zimetulia kwahiyo ishu ni kwako kuamua ipi inafaa.
Bei kwa K7 unaweza kupata kuanzia Laki Mbili huku K9 unaweza kupata kuanzia Laki Tatu na kuendelea.
Tags
# Teknolojia
# Uchambuzi
Share This
About Swahili Muzik
Uchambuzi
Labels:
Teknolojia,
Uchambuzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.
No comments:
Post a Comment