Kuna maajabu mengi Duniani na mojawapo ni hili la Taa ambayo inashikilia Rekodi ya kuwaka kwa muda mrefu zaidi.
Unaambiwa Balbu hiyo inawaka kuanzia mwaka 1901 na inapatikana huko LIVERMORE, CALIFORNIA ambapo kitengo cha Zimamoto kutoka Livermore ndiyo wamepewa mamlaka ya kuitunza na ndipo inapopatikana.
Kwa mwanzo Balbu hiyo inasemekana ilikuwa ikitoa Watt 40 mpaka 60 lakini kwa sasa inatoa Watt 4 Tu. Kutokana na Historia inasema kuwa Taa hiyo ilitengenezwa na kampuni ya Shebby Elecric ambapo unaambiwa Taa nyingi zilizotengenezwa na Kampuni hiyo kwa miaka ya Zamani mpaka sasa Zinafanya Kazi.
SOMA PIA>> WASANII HAWA HAPA UTAWAPATA KATIKA ALBAMU MPYA YA DIAMOND
Zylpha Bernal Beck anasimulia kuwa Taa hiyo ilitolewa na Baba yake kwa kitengo hicho cha kupambana na moto mwaka 1901 ikiwa ni kama msaada.
Taa hiyo iligundulika mwaka 72 na ripota aliyefahamika kwa jina la Mike Dustan ambae alifanya mahojiano na watu walioishi eneo hilo kwa muda mrefu ambapo baadae aliamua kuwaita watu wa Guinness Records ambao badae walithibitisha kuwa Balbu hiyo ndiyo ambayo imewaka kwa muda mrefu zaidi.
Kwanini Inawaka kwa Muda mrefu?
Baadhi ya tafiti zilionesha kuwa kuwaka kwa Balbu hiyo kwa muda mrefu kunatokana na namna material yake yalivyotengenezwa ambayo kwa kiasi kikubwa hulinda Vacuum kwa lugha rahisi ile glassi yake isipoteze uga wake ambao ndiyo huwa chanzo kwa balbu nyingi kuzidiwa na kupasuka.
Balbu hiyo hutembelewa na watu wengi na kwa sasa kuna kitengo maalumu kiliundwa kwaajili ya kuilinda Taa hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.
No comments:
Post a Comment