Ay: Mashabiki Bongo Wanatuchezea Sana - teknomovies
Ay: Mashabiki Bongo Wanatuchezea Sana

Ay: Mashabiki Bongo Wanatuchezea Sana

Share This
“Upo Hapo” ndio ngoma ambayo imewakutanisha Manguli watatu wa Hip Hop ya Bongo Ay,Mwana Fa pamoja na Fid Q ambayo inaendelea kukimbiza kwa sasa katika vituo mbalimbali vya Redio pamoja na Luninga.
Akiongelea ngoma hiyo Ay anafunguka kuwa ujio wa ngoma hiyo ilikuja kama kiutani utani kwa sababu wao ni marafiki ambao mara nyingi wanakuwa pamoja.

“Siku zote huwa nafanya kazi na Mwana Fa,Lakini nikaona kwanini kwa sasa tusiongeze ladha nyingine ya tofauti na wote kwa mwanzo tulikuwa na wasi wasi kama itaenda kama inavyotakiwa,”
“Lakini baada ya kuachiwa hata Fid Q mwenyewe kaona mafanikio yake yamekuja makubwa sana naweza kusema zaidi hata tulivyotegemea,”

Wazo la wimbo

“Mara ya kwanza Mwana Fa alikuja na wazo la jina na pia korasi,aliponiambia nikaona imetulia hivyo biti lilianza kutengenezwa na kitu kikafanyika fasta,”

Mafanikio ya Uzinduzi ya video.

Kwa sasa ni nadra sana kuona uzinduzi wa video,lakini kwa upande wao waliamua kufanya uzinduzi ambapo Ay anafunguka kuwa hiyo imewasaidia kwa kiasi kikubwa na kuongeza kuwa wana mpango wa kufanya pia hata sehemu zingine.

“Sio hapa tu,mpaka nje ya nchi tuna mpango huo alafu hizi vitu zina faida sana kwa sababu una kutana na watu mbalimbali,unapanua zaidi mtandao kwa hiyo inasaidia kwa kweli,”

Mpango wa kundi vipi

“Hata sisi bhana tunawaomba wadau watuombee liwe kundi,lakini unajua kwa sisi inakuwa kazi kidogo kwa sababu kila mtu ana mipango yake alafu tumeanza tangu muda kila mmoja akifanya kazi kivyake,”

“Mimi nina nyimbo nyingi nimefanya na Fid Q pamoja na Mwana Fa,hatuwezi kujua mipango ya baadae lakini tutajua zaidi,”alisema

Wazo la video

“Kuhusu wazo alikuwa ni Fid Q pamoja na Mwana Fa walikuja na wazo jinsi itavyokuwa na muongozaji aliipenda,ikaongezewa nyama kadhaa mwisho wa siku imetokea kama mnavyoona,”

Vipi kuhusu makolabo ya nje

Ay ni moja wa wasanii wa mwanzo kibongo bongo kufanya kolabo na wasanii wa nje,mfano kama kolabo yake na P Square,Miss Triniti,Sean Kingston ambazo ziliweza kufanya vizuri.

Lakini kwa miaka kadhaa amepunguza kuachia kolabo hizo ambapo anafunguka kuwa,kolabo hizo anazo za kutosha tatizo ni muda sahihi.

“Zipo kolabo za kutosha sana,nimefanya na akina Ray J,Busta Rhymes lakini tatizo huwa naziona kama sio za wakati huu,”

“Na pia mimi kufanya kolabo na wasanii wa nje huwa napata kikubwa ni uzoefu tu ila kolabo zipo naangalia kwa sasa muda sahihi ili nisije kuachia alafu ikaishia hewani tu,”

Mtazamo wake kwa Muziki wa sasa

Muziki wa sasa umekuwa wa kubadirika badirika sana, ambapo Ay anaongeza kuwa wanaosababisha hilo kwa asilimia kubwa ni mashabiki.

“Siku zote msanii huwa anaangalia mahitaji ya mashabiki,mfano unakuta watu wanalalamika mbona nyimbo za mapenzi zimezidi sana,lakini wanasahau kuwa wao ndio wanaosababisha nyimbo hizo zizidi kuongezeka,”

“Mashabikii ni kama wanakuwa wanatuchezea hivi kwa hiyo kwangu kubadirika badirika kwa wasanii ni jambo la kawaida na Muziki naona unakua sana tu,”

Mipango ya Albamu.

“Mipango ya Albamu naweza kufikiria kama Kampuni ya usambazaji itakuja na mipango mizuri na ambayo inaeleweka vizuri,”

“Mimi nilikuwa mtu wa kwanza kusema sitoi albamu,watu wakaona nazingua lakini kwa sasa unaona kila msanii akafuata hivyo kama Albamu watu wanataka zirudi tena,njia kuu ni kampuni ya usambazaji ambayo itafanya kazi hiyo kuja na mipango sahihi na wazi,”

“Kwa sababu haiwezekani,mtu anakusambazia kazi zako alafu anakosa rekodi sahihi,yani hajui mkoa gani ambao kopi zangu zimeuza sana na sehemu fulani sijauza vizuri,”

“Kwa sababu kwa wenzetu nje ipo utasikia msanii kama Lady Gaga mfano kauza kopi kadhaa na bara fulani kopi zake ndio zimeuza vizuri zaidi,yani ni kitu kidogo tu cha kufanya na hakihitaji nguvu kubwa ni kupangilia tu,”

Mipango ya kusaini wasanii.

Kuna kipindi ambacho Ay alikuwa akiwasimamia baadhi ya wasanii kama Stereo pamoja na Ommy Dimpoz ambapo kwa sasa wapo sehemu nyingine.
“Unajua kwanza Stereo ulikuwa ni mkataba wa mwaka mmoja na pia sikumuacha Stereo watu wajue hilo kwa sababu bado nafanya nae kazi,naendelea kumpa ushauri wa hapa na pale mfano kolabo yake na Rich Mavoko mimi niliongea na Diamond,”

“Hata Rich Mavoko kusaini Wcb,nilimwambia Diamond afanye kumsaini ni msanii mzuri,lakini hii kwa wasanii wengi mimi nafanya hivyo kama kuunganisha pia kuna baadhi ya wasanii wanaokuja Bongo na pia hata wanaoenda nje kama kufanya shoo huwa napanga mipango kadhaa sababu mapromota huwa wananicheki,”

Bonyeza HAPA kushusha Wimbo Huo pamoja na Kutazama Kichupa Kizima Kama Bado.


Pages