Polisi nchini Israel imemkamata kijana mmoja mwenye asili ya Palestina kwa kosa la kuandika "Good Morning" kwa kiarabu kwenye mtandao wa Facebook.
Kijana huyo ambae jina lake limehifadhiwa amekamatwa na Polisi baada mtandao wa Facebook kushindwa kutafsiri neno la Kiarabu la Asubuhi Njema na kutafsirika "Washambulie hao" kwa lugha ya Kiyahudi.
Kwa mujibu wa maelezo ya polisi kutoka Judea na Samaria nchini Israel inaeleza kuwa kijana huyo ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi na aliposti picha hiyo akiwa katika maeneo ya West Bank.
Polisi wameeleza kuwa baada ya kuona posti hiyo walichukua uamuzi wa
kumsaka kijana huyo na kumkamata ndani ya masaa matatu ili kumuhoji
kuhusu kauli yake iliyotafsiriwa kama ni ya kichochezi.
SOMA PIA:MAKALA KUMUHUSU ROSA REE
Hata hivyo masaa machache baada ya mahojiano aliachiwa huru na polisi
baada ya kupata msaada kutoka kwa mtalaamu wa Lugha aliyetafsiri kwa
ufasaha neno hilo la ‘Goood Morning’ kwa lugha ya kiyahudi.
Facebook imekuwa ikilaumiwa na watu wengi wanaotumia lugha mbalimbali
duniani kwa kushindwa kutafsiri kwa ufasaha baadhi ya maneno kutoka
kwenye lugha husika.
Kwa upande mwingine Polisi wamesema walipatwa na hofu kubwa kwa
kumuona kijana mwenye asili ya Palestina akiandika ujumbe huo uliokaa
kichochezi huku akiwa karibu na Tinga Tinga.
Ambapo eneo hilo hilo miezi
miwili iliyopita kulitokea tukio la kigaidi baada ya watu waliosadikika
kuwa ni magaidi waliendesha Tinga Tinga kwenye umati wa watu na
kujeruhi watu wawili.
Nchini Israel hakuna polisi wa kutosha wanaojua kiarabu kwa ufasaha hivyo mara nyingi matatizo kama hayo hutokea.
Source: Csoonline.com
Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali lakini pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.