Google
play ni moja kati ya Soko kubwa la kushuusha App nyingi za bure na za
kununua. Soko hili hutumiawa na watumiaji wa vifaa vya Adroid japokua hata kwa
kompyuta yako unaweza kuingia katika soko hili sema ni vigumu kushusha App.
Google play ndio soko linaloongoza kwa App za bure ukiachana na masoko mengine
kama lile la AppStore linalomilikiwa na Apple Inc.
Soko la Google Play kama jina lake lilivyo linamilikiwa na
kampuni ya Google, sasa ili kujua mbinu tofauti kuhusiana na soko hili endelea
kusoma zaidi
A: FUATILIA SIMU ILIYO POTEA AU KUIBIWA
Ndio unaweza kufuatilia simu yako iliyopotea au kuibiwa lakini
simu yako ya Android inabidi iwe na vitu muhimu vitatu ambavyo ni
- Kifaa chako kiwe kimeunganishwa na akaunti yako ya
google
- Kifaa chako lazima kiwe na uweza wa kuingia katika
mtanadao (ineternet)
- Lazima kifaa chako kiwe kimewasha sehemu ya ‘Location
Settings’
Kama simu yako imekidhi hayo mambo yote hapo juu, basi tunaenda
sawa. Sasa fungua mtandao wa ‘Android
Device Manager‘ – https://www.google.com/android/devicemanager na
kisha anza kufuatilia simu yako iliyopotea au kuibiwa ili kujua ipo eneo gani
kwa kutumia ramani.
B: FUTA DATA ZAKO ZOTE KWA KUTUMIA GOOGLE PLAY
Hii ni moja kati ya zile mbinu nzuri tuu unazoweza fanya ukiwa
na kifaa chako cha Android. Kwa kutumia njia hii unaweza uka RESET
skifaa/simu yako ya android lakini kifaa hiko lazima kiwe na mambo mawili ya
muhimu
- Hakikisha kina uweza wa kimtandao (internet)
- Hakikisha kifaa chako kimeunganishwa na akaunti ya google
Kama una uhakika kifaa chako kimekidhi mambo yote hayo basi
nenda katika ‘Android Device Manger‘ kisha futa kila kitu katika simu
yako iliyoibiwa au kupotea. Hii itahakikisha usalama wa vitu vyako (mfano
Picha, nyaraka, video na mafaili mengine ya muhimu) ndani ya kifaa. Kwa
Njia 3 za Ku Reset simu ya Android soma Hapa
C: RUDISHIWA KIASI ULICHOTUMIA KUNUNUA APP USIYOIPENDA
Hivi umenunua App ambayo baadae haifanyi kazi kama ulivyodhani
au hukuipenda na akajuta kupoteza hela yako bure?. Sasa unafanyaje?
Google hurudisha kiasi ulichotumia kwa App ambazo hazifanyi kazi
kama ulivyotegemea lakini kwa zoezi hili kukamilika kuna vigezo na masharti
ambayo inabidi yazingatiwe.. zoezi
hili litafanyika mara moja tuu kwa kila App hivyo usije
kujisumbua kuomba kurudishiwa kiasu chako zaidi ya mara moja.
Kitu kingine ni kwamba unaweza omba kurudishia kiasi chako baada ya masaa mawili kupita tangia ulivyo nunua App hiyo. Ili kurudishiwa kiasi chako, fungua Google play store na itafute hiyo App ya kulipia uliyoishusha. Ikishatokea ataona sehemu imeandikwa ‘REFUND’ bofya juu yake na Google ita rudisha kiasi hicho ndani ya masaa 48. Kitu kingine kizuri kuhusu hii ni kwamba hakuna sera ya maswali kwa hiyo unaweza omba kurudishiwa kiasi chako. Hii inamaanisha huwezi kuulizwa maswali mia ili kurudishiwa kiasi chako.
Kitu kingine ni kwamba unaweza omba kurudishia kiasi chako baada ya masaa mawili kupita tangia ulivyo nunua App hiyo. Ili kurudishiwa kiasi chako, fungua Google play store na itafute hiyo App ya kulipia uliyoishusha. Ikishatokea ataona sehemu imeandikwa ‘REFUND’ bofya juu yake na Google ita rudisha kiasi hicho ndani ya masaa 48. Kitu kingine kizuri kuhusu hii ni kwamba hakuna sera ya maswali kwa hiyo unaweza omba kurudishiwa kiasi chako. Hii inamaanisha huwezi kuulizwa maswali mia ili kurudishiwa kiasi chako.
D: PATA ORODHA YA APP ZAKO ZA ZAMANI
Umeuza kifaa chako cha Android hivi karibuni na unataka orodha
ya App ulizokuwa unatumia hapo awali? Google inakusaidi katika hilo, ‘Sign In’
katika Google Play kwa kutumia Akaunti yako ya kwanza kisha nenda Apps > My Apps ili
kupata orodha ya App zako zote ulizowahi kushusha kwa sababu google inahifadhi
App zote ulizowahi shusha