INSTAGRAM siku hizi ndo imekua sehemu ya watu wengi maarufu
kutolea mapovu yao mengi pengine inaweza ikawa sababu ya umaarufu wa mtandao
huo na uwepo wa watu wengi wanaotumia pia.
Majuzi kolabo hatari ambalo liliingia doa mapema,kati ya Idris
Sultan na Wema Sepetu lilianza kuonekana tena kuanza kurudi rudi baada ya wote
kwa pamoja kutokea wakiwa pamoja katika usiku wa uzinduzi wa Filamu ya wema
sepetu.
Lakini si muda hali ilichafuka baada ya Idris kuzindua viatu vyake ambapo Wema yeye hakutokea ambapo mwanadada Wema aliweza kutoa povu zito katika Instagram yake akiomba msamaha kwa kitendo hicho.
Wema katika post hiyo anasema jambo kubwa lililosababisha
kukosekana katika sherehe hiyo ni kutokana na nguo aliyotakiwa kuvaa kuharibiwa
hivyo kushindwa afanye nini.
Wema anadai Idris hapokei simu yake hivyo kaamua kuomba
msamaha kwa njia hiyo ambayo anaona ingeweza kumfikia vizuri na kweli
iliwezekana sababu ni kama mashabiki wa Wema walihamia kwenye ukurasa wa Idris
wakimuombea msamaha kipenzi chao.
Idris katika mahojiano na Teknomovies Blogu anasema yeye hana noma na
ashapotezea jambo hilo.
“Sina noma yoyote, nishapotezea sababu ni mshikaji, kitu cha
kawaida tu,”
Alipoulizwa juu ya suala la kumpenda bado Wema, Idris alikataa
kujibu swali hilo na kasha kupotea angani.
“Hilo swali naomba nilitunze tu kwanza,” alimaliza.
No comments:
Post a Comment