Hatua 10 Za Kufanya Urudiane Na Ex Wako - teknomovies
Hatua 10 Za Kufanya Urudiane Na Ex Wako

Hatua 10 Za Kufanya Urudiane Na Ex Wako

Share This
Kuachana na mpenzi wako ni kitu cha kawaida watu hupitia kila siku. Aidha inawezakuwa mumeachana kwa sababu ya kukosana, kutoaminiana, kusalitiana na sababu nyingine nyingi ambazo unazijua wewe.

                                    
Aidha, unaweza kukosana na mpenzi wako kwa kosa dogo sana mpaka ukawa unajiuliza maswali ni kwa nini ama ni kitu gani kilichofanya ukosane na mpenzi wako. Wengine inafikia mahali wanatamani kurudiana na wapenzi wao.

 Leo tumeona ni bora zaidi tuwasaidie ndugu zetu ambao wanataka kurudiana na ex wao.

Enyewe inaweza kuwa ngumu unapoachana na mpenzi wako haswa ukizingatia yale mambo yote mazuri ambayo mumekuwa mkifanya mkiwa pamoja. Vile vicheko, tabasamu, saprizes, nk inasisimua.

So utafanyaje urudiane na ex wako? Mbinu zenyewe za kufuata ndizo hizi:

#1 Mtumie Ex wako SMS.  Kila kitu huanza na hatua ya kwanza. Mtumie ujumbe wa kawaida tu. Si lazima uandike jumbe ndefu ambayo inaweza kumuuliza kichwa. Unaweza kumtumia jumbe ‘Habari za masiku’. Hapa anaweza kukujibu kinjia mbili. Anaweza kuwa na jibu chanya au hasi. Jibu chanya ni majibu ambayo ni kuonyesha ameridhika kwa kumjulia hali. Anaweza kujibu, ‘Asante kwa kunijulia hali, unaendeleaje?’. Hakikisha humtumii jumbe wakati wote. Jumbe mbili-tatu zinatosha kwa siku. Mwache yeye aanze aproach.

#2 Nenda polepole bila pupa. Kurudiana na Ex wako kunahitaji hatua ya polepole. Hii ni kumaanisha usiingize hisia za mapenzi kwayo. Unataka urudiane na Ex wako hivyo lazima uende na spidi yake. Usiende mbio wakati breki anaikontroli yeye. Pia iheshimu himaya binafsi yake. Ukiwa unaongea naye ana kwa ana weka nafasi kati yako na yeye.

#3 Mpigie simu mara kwa mara. Mpigie simu mara kwa mara. Lakini kama nilivyotangulia kusema katika hatua ya kwanza usiwe na pupa. Usimpigie kila lisaa. Anza kwa kumpigia mara moja kwa siku/mbili. Halafu punguza  huo muda pole pole mpaka iwe mazoea ya kumpigia simu. Hii itakuwa na mpigo mkuu kufufua hisia zenu.

#4 Mwambie kuwa unammiss. Mwambie unammisi. Yafanye mazungumzo yenu yawe sahili mwanzo mwanzo. Usimpresha na mambo mazito. Usimkumbushe mambo ambayo yalichangia kwenu kuachana. Tayari anajua. So wewe makinika na kumwonyesha kuwa unamisi uwepo wake kwako. Hakikisha hukumbushi matukio yaliyochangia kuachana kwenu.

#5 Fanya yale mambo madogo madogo. Kufanya mambo madogo madogo kunachangia kuleta mabadiliko. Kwa mfano akitaka usaidizi mdogo wewe unajitokeza unamsaidia bila kuitisha chochote.

#6 Makinika na hisia chanya zenu za awali. Zungumza yale mambo mazuri mliokuwa mnapitia pamoja. Mambo ambayo yaliwafanya mkawa kitu kimoja. Hakikisha kuwa unaepuka kuzungumza mambo yeyote mabaya. Hisia chanya kutachangia kufufua chembechembe zozote za mapenzi ambazo alikuwa nazo.

#7 Tangamana na marafiki wenu wa awali. Kama ameamua kutoka out, hakikisha unatoka na marafiki wenu wa awali. Hakikisha hauzui hisia zozote. Tembea na yeye bila kuwa na hisia zozote. Mchukulie kama rafiki yako tu.

#8 Usizungumzie maisha yako baada ya kuachana. Usijaribu kuyafananisha maisha yako ya sasa na yale ya awali. Usiongee kuhusu maisha yamekuwa magumu ama mazuri tangu uachane na yeye la sivyo utaongeza chumvi ndani ya kidonda.

#9 Usimuombe. Kosa ambalo wengi hufanya ni kumpigia Ex wake magoti na kumwomba warudiane. Ukifanya hivi utakuwa unampa ishara ya kuwa wewe  huwezi kujitegemea kivyako hivyo kumfanya akutenge zaidi. Unachotakiwa kufanya ni kuonyesha confidence.

#10. Enjoy romance. Baada ya kuwasiliana, kumweleza hisia zako na kuingiliana, sasa hapa una nafasi ya kuendeleza romance kama kawaida. Ukifuata mbinu tulizoziorodhesha awali vizuri basi kila kitu kitakuja natural.

Ok. Hizi ndizo mbinu za kufuata kumrudisha Ex wako. Lakini kabla kuchukua hatua hii unapaswa kwaza kujiuliza ni kitu gani kilichochangia nyinyi wawili kuachana. Na je, ukirudiana naye hamtakosana tena?

Pages