Mjue Vizuri Huyu Jamaa,Mkali Wa Into The Badlands - teknomovies
Mjue Vizuri Huyu Jamaa,Mkali Wa Into The Badlands

Mjue Vizuri Huyu Jamaa,Mkali Wa Into The Badlands

Share This
Sura hiyo wengi walioona kwenye Into the badlands, lakini kiukweli jamaa kafanya michongo mingi sana sana, sema katika michongo iliyopita watu wengi hawakumpa attention sana ya kutaka kumjua kama alivyoonekana katika Into the badlands.

Jina lake kamili anaitwa Marton Paul Ckosas, siku yake ambayo alitokea duniani kwa mara ya kwanza ilikua ni tarehe 30 june mwaka 1966, Akikulia katika kitongoji cha Invercagirll huko New Zealand.

Mama yake alikua ni Nurse na Baba yake alikua Mechanical Engineer, Huku Baba yake akiwa na asili kutoka Hungary na mama yake Akiwa na asili ya Kiingereza, ki Irish na pia ki Danish na ndomana Lafudhi ya Marton kama mnavyo iona ipo tofauti kidogo. Ana mdogo wake anaefahamika kwa jina la Robert, Marton ana uraia wa nchi mbili mpaka sasa..Uraia wa Hungary na pia New Zealand.

Kazi rasmi ya uigizaji alianza tangu mwaka 1990, akianza kutokea, katika Series ya Shark in the park, badae alitokea katika series nyingine kwa episode moja ya katika Series nyingine inayokwenda kwa jina la Technical K.O.

Kutoka mwaka 1993 mpaka mwaka 1995 alicheza katika Soap Opera inayokwenda kwa jina la Shortland Street.

Mwaka 1997 alitokea katika movie ya mapenzi, iliyokwenda kwa jina la Broken English, pia toka mwaka 1997 mpaka mwaka 2001 alicheza katika series inayokwenda kwa jina la Xena:Warrior Princess akicheza kama Xena , pia alicheza vyema katika The Lord of the Rings: TheFellowship of the Ring mwaka 2001 na mwaka 2003 pia katika The Lord of the Rings: The Return of the King.

Katika lord of the rings Filamu

Mwaka 2002 pia alicheza kama jambazi kuu katika XxX pia bila kusahau katika The Bourne supremacy alisababisha vyema sana. Mwaka 2007 alionekana pia katika series ya Romulus, My Father ambapo ilimpa tuzo mbili kama best supporting actor.

Katika Bourne supremacy 
Alitokea katika movie pia ya Alice in Wonderland hiyo ilikua mwaka 2010.
Kwa mwaka 2014 alitokea katika michongo mikali kama The Amazing Spiderman 2 na pia The Equalizer, akiwa sambamba na mtu mzima Denzel Washington.
Katika The equalizer 

Na mwaka 2015 ndio mwaka ambao aliingia rasmi katika series inayopendwa sana na watu ya Into the badlands.. Na kwa mwaka 2017 pia kuna movie ambayo ishakwisha toka inayokwenda kwa jina la voice from the stone akiwa pamoja na mdada aliyejipatia umaarufu toka Game of thrones akifahamika kwa jina la Emilia Clarke.
Hiyo ni story fupi ya mtu mzima Quinn, na baadhi ya movie ambazo anapatikana, najua zingine utakua umestuka ni kama hukumuona kumbe ndo yeye.


Source: Wikipedia na Vyanzo Mbalimbali.

Pages