Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Vikonje A wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamezichapa kavukavu wakigombea TZS 100,000 iliyotolewa na Rais Dkt Magufuli wanunue soda.
Rais Dkt Magufuli alitoa fedha hizo kwa wakazi hao wa kijiji kilichopakana na Ikulu ndogo ya Chamwino aliposimama kuwasalimu wakati akiwa njiani kuelekea kwenye makaziyake.
Mwenyekiti wa Kitongoji hichoalisema jana kuwa, alipopokea fedha hizo aliwapa wanaume 40,000 na wanawake kiasi hicho hico huku 20,000 akiielekeza kuchangia ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo. Kiongozi huyo alisema kuwa, ugomvi uliibuka upande wa wanaume ambao baadhi walitaka mgao mkubwa kuliko wengine.Licha ya kuwa kiongozi huyo aligawa fedha hizo watu wakiona na kumpa Diwani 20,000 ya mchango wa shule, baadhi ya watu walimtuhumu kuwa amezichukua kwa ajili yamatumizi yake binafsi.Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kitongoji, Robert Mshana aliwataka wakazi wa Kijiji hicho kubadilika kwani eneo hilo litakuwa eneo muhimu kutokana na Ikulu ya nchi kuhamia hapo.Mshana aliyasema hayo wakati wa kikao cha kijiji kilicholenga kuwaelimisha wanakijiji juu ya mipaka ya Ikulu ya Chamwino na kuorodhesha mali zao ili waweze kulipwa fidia kupisha upanuzi wa Ikulu.
-Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.
No comments:
Post a Comment