MAREKANI YAPIGA MARUFUKU KUINGIA NA LAPTOP NDANI YA NDEGE KAMA UNATOKA KATIKA NCHI HIZI. - teknomovies
MAREKANI YAPIGA MARUFUKU KUINGIA NA LAPTOP NDANI YA NDEGE KAMA UNATOKA KATIKA NCHI HIZI.

MAREKANI YAPIGA MARUFUKU KUINGIA NA LAPTOP NDANI YA NDEGE KAMA UNATOKA KATIKA NCHI HIZI.

Share This
Marekani imetangaza kupiga marufuku vifaa vya umeme hususan Laptop na Tablet kuingia navyo ndani ya ndege kutoka katika nchi 8 za Mashariki ya kati na Afrika Kaskani ambazo wamezitangaza. Sheria hiyo inaanza kufanya kazi mara moja.

Sheria hii itatumiwa na ndege zinazotoka katika miji ya Cairo (Misri), Amman (Jordan), Kuwait City (Kiwait), Casablanca (Morocco), Doha (Qatar) Riyadh na Jeddah (Saudi Arabia), Istanbul (Turkey) na Abu Dhabi.



Abiria hawataruhusiwa kuingia na Laptop, Tablet na Camera ndani ya ndege na badala yake vifaa hivyo vitawekwa eneo la mizigo isipokuwa Abiria anaweza kuingia na simu

Pia sheria hii haitamuhusu Mmarekani anaetoka katika nchi hizo na badala yake ni wale ambao si wamarekani wanaotoka katika nchi hizo.

Rais Trump anachukua hatua hizi kama njia ya kupunguza ugaidi.


No comments:

Post a Comment

Pages