Mambo 5 ya kufanya kipindi hiki cha mwisho wa mwaka - teknomovies
Mambo 5 ya kufanya kipindi hiki cha mwisho wa mwaka

Mambo 5 ya kufanya kipindi hiki cha mwisho wa mwaka

Share This
Mwaka 2017 unakwisha, zimesalia siku kadhaa tuumalize rasmi. Mwezi wa 12 (December) ni mwezi mzuri wa kufanya tathmini kwa yale yote ambayo umeyafanya kuanzia January.


.Mtandao wa teknomovies.com umekuandalia mambo sita ya kufanya kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ili uweze kuupokea mwaka 2018 ukiwa na nguvu mpya kabisa.

 1. Fanya tathmini kwa yote uliyofanya mwaka 2017

Hili ni jambo muhimu kabisa la kufanya kwa kipindi hiki. Chukua muda wa kutosha, kaa peke yako kisha yapitie yale yote uliyoyafanya mwaka huu. Je yalikuwepo kwenye mipango yako? Umeyatimiza? Umejifunza nini kupitia jambo/mambo hilo/hayo?. Majibu ya maswali haya yatakupa sura mpya kwa mwaka 2018.

2. Toa shukrani kwa uwapendao 




Shukrani ni tendo dogo kulifanya lakini ni hazina kubwa. Familia na marafiki ni makundi yenye ufunguo wa mafanikio yako. Tenga muda kuwashukuru kwa yote yaliyotokea kwa mwaka 2017

3. Tembelea sehemu mpya 

Kuanzia January hadi November ni mara chache sana mtu kupata nafasi ya kutembelea sehemu na kupumzika lakini mwisho wa mwaka ni muda wa kufanya matembezi kwa sehemu ambayo itakufanya ufarahie  kwa kuitembelea kwa mara ya kwanza.


4.  Jifunze jambo jipya

Bado hujachelewa unaweza kujifunza jambo jipya ambalo litakufanya uanze mwaka 2018 ukiwa na kitu cha ziada kwenye fikra yako. Usihofie kujifunza kitu kipya kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwka,

5. Tengeneza ramani ya mwaka 2018

Hili ndilo jambo muhimu kabisa kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka. Hakikisha unaanda mpango mkakati ambao utautekeleza kwa mwaka 2018


Kampuni ya Dollars Media Group wamiliki wa mtandao wa teknomovies.com inakutakia heri na nafaka kwa mwaka 2018...Tunakushukuru kwa kuwa nasi kwa kipindi chote cha mwaka, tunakuahidi mambo mazuri 2018.

Creativity is Our Priority 

No comments:

Post a Comment

Pages