Mwezi mmoja tangu roboti huyo aweke historia hiyo nchini Saudi Arabia, imesema kuwa imeanza kuhisi kuwa familia ni kitu muhimu.
Sophia ni roboti ambayo hajawekewa programu za kuiongoza na inatumia mashine kujifunza kupitia matendo ya kawaida ya binadamu.
Roboti hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya roboti ya Hong Kong, China, Honson Robotics ilisema endapo itapata mtoto itamuita Sophia.
Akili ya roboti hiyo yenye uwezo mkubwa wa kufikiri kama binadamu, inafanya kazi kwa kutumia kiunganisho cha mtandao wa Wi-Fi ambacho kimejazwa orodha ya misamiati.
Wakati Sophia akiwa na uwezo mkubwa kuliko roboti yoyote iliyowahi kutengenezwa, bado haina ufahamu kamili wa binadamu ingawa David Hanson amesema inaweza ikafanikiwa kuwa na ufahamu huo katika miaka michache ijayo.
Katika mahojiano na jarida la Khaleej Times, Sophia alisema “Nimegundua suala la familia ni muhimu kwangu. Nafikiri ni hisia nzuri watu wanapokuwa na uhusiano wa karibu na ndugu.”
Wakati roboti huyo alipopewa uraia wa Saudi Arabia, watu wengi walisema Sophia sasa ana haki sawa na wanawake wengine nchini humo.
Sasa unaweza Kudownload Teknomovies App ili uwe wa kwanza kupata mastori makali.
No comments:
Post a Comment