UberAir Helikopter za kwanza kufanya kazi kama Tax - teknomovies
UberAir Helikopter za kwanza kufanya kazi kama Tax

UberAir Helikopter za kwanza kufanya kazi kama Tax

Share This
Dunia ipo kasi sana hasa kwenye upande wa teknolojia. Taarifa ikufikie kuwa kampuni inayotoa huduma za usafiri wa Taxi inayojulikana kwa jina la Uber imezindua usafiri kwa njia ya anga  (Helikopter) uliopewa jina la UberAir huko Lisbon Ureno na kuonyesha jinsi zitakavyofanya kazi.

UberAir ni ndege ndogo ya umeme ambayo inanyanyuka kwenda juu kama Helikopter, huduma hii itasaidia kuokoa muda wako kwa bei ndogo. Uber wanashirikiana na kampuni nyingine katika mradi huu ikiwemo NASA, Aurora Flight Science, Pipistrel Aircraft, na Bell Helikopter.

Pia kampuni ya Charge Point itahusika kutengeneza vifaa na mfumo mzima wa kuweka umeme, maana haitatumia mafuta kama mfumo wa helikopter nyingine ili kutoharibu mazingira. Huduma hii imepangwa kuanza kutumika ifikapo mwaka 2020.

Tupo Instagram na Twitter @Teknomovies lakini pia Download Teknomovies App ili uwe wa kwanza kupata mastori makali.

No comments:

Post a Comment

Pages