Katika list ya Filamu zangu bora kwa upande wa sayansi za
kufikilika (Science Fiction) Iron Man ni filamu ambayo haiwezi
kukosa katika list yangu.
Ubora wa filamu haufichiki hasa kutokana na ubora wa uhusika
wa Tony Stark (Robert Downey Jr)
ambae ameweza kuifanya filamu kuvutia sana.
Lakini kuna mengi watu huwa hawajui juu ya uhusika wa Tony Stark ambao umejengwa katika
filamu ebu ngoja nikufahamishe fasta kuanzia kumi mpaka moja.
10. Ilichukua miaka 20 kufanyika kwa filamu ya kwanza ya Iron
Man.
Kuanzia mwaka 1999 ndipo wazo la kufanyika kwa filamu
lilipangwa lakini haikufanikiwa kufanyika. Tena mwaka 2001 mipango ilianza
kufanyika lakini haikufanikiwa tena.
Inasemekana katika mipango hiyo waigizaji kama Tom Cruise na Nicolas Cage walikuwa wanategemewa kucheza kama Tony Stark.
9. Ni moja ya
waanzilishi wakubwa wa The Avengers.
Wengi mmetazama filamu hiyo ambayo imejaa watu hatari kama The
Hulk,Captain America,Thor ambao kihistoria inaonesha kuwa mtu aliyeunganisha
timu hiyo ni Tony.
Na hata makao makuu yao yalikuwa katika nyumba ya
Tony,Usisahau kuwa Jamaa katika filamu ni moja ya mabilionea hatari na
wanaopendwa na wengi hasa mabinti.
8. Alifundishwa ngumi
na Captain America.
Unaweza ukashangaa lakini huo ndo ukweli ki filamu filamu.
Hili lilikuwa linafahamika wazi kuwa Tony bila kutumia suti yake kiuhalisia ni
mtu wa kawaida tu. Lakini baada ya muunganiko wa Avengers alikuwa akifundishwa
ngumi na Camptain mwenyewe kwamba endapo hali ikibadilika aweze kupambana hata
bila kuwa na suti yake.
7. Tony ana Masters
degree ya mambo ya Fizikia pamoja na Engineering alipata akiwa na miaka 17 tu
Hiyo kifilamu filamu,Akiwa na miaka 16 alienda kusoma katika Massachusetts
Institute of Technology na miaka miwili mbele alimaliza akiwa na master yote
kutokana na U genius wake.
6. Anamiliki “Area 51”
Jamaa ni tajiri sana,hivyo aliamua kununua Area 51 ambayo makazi kwa watu hayaruhusiwi na ni eneo
kwaajili ya majaribio ya kijeshi. Hivyo yeye alinunua kwa shughuli zake
mwenyewe japokuwa katika filamu hatujawahi kuoneshwa sana namna lilivyotumika
5. Ili Kujiandaa na role ya Iron Man, Robert Downey Jr
alitumia siku tano kufanya mazoezi ya nguvu kwaajili ya kujiweka mwili wake
fiti kwaajili ya role hiyo iliyomtaka kuwa na mwili stahiki kuendana na
muhusika Tony
4. Iron Man ndio filamu pekee ya kwanza Marvel kutumia mpunga
wao wenyewe bila kusaidiwa na kampuni nyingine yoyote.
3. Unaweza kutengeneza Suti ya Iron Man ukiachana na kama kuwa
ya kufikirika. Tafiti zinasema unahitaji kiasi cha gharama kama $80,000 na
ujuzi mkubwa katika masuala ya Engineering
2. kama sio Robert Downey Jr basi tungemuona Tom cruise ambae
kampuni kwa kiasi kikubwa ilitaka nae kucheza role ya Tony Stark
1. Ni tajiri mkubwa sana
ambapo anashikilia namba 36 katika list ya matajiri duniani lakini kumbuka hiyo ni ki filamu filamu tu na si ki maisha halisi.
No comments:
Post a Comment