Youtube Yatangaza kuwawekea Ngumu Watu Hawa - teknomovies
Youtube Yatangaza kuwawekea Ngumu Watu Hawa

Youtube Yatangaza kuwawekea Ngumu Watu Hawa

Share This
Youtube imetangaza kuzidi kuwawekea ngumu watu wenye misimamo mikali ambao wamekuwa wakichapisha video zenye maudhui ya kuhamasisha misimamo mikali katika mtandao huo.
Hatua hii imekuja baada ya mtando huu kuendelea kukosolewa kwa kutodhibiti watu wenye msimamo mkali katika mtandao huo.

Watu wenye misimamo mikali ya kibaguzi kidini na kiimani wamekuwa wakitumia mtandao huu kueneza misimamo yao, hili limepelekea matatizo mengi pamoja na ugaidi wa kisasa ambapo mtu haitaji kwenda mahali fulani kuwa na msimamo mkali bali ni kompyuta na intaneti tu.

Kwa muda mrefu serikali za nchi mbalimbali zimekuwa zikihimiza mitandao (Youtube ikiwemo ) kufanya jitihada kuzuia misimamo mikali, kwa upande wao Youtube wamekiri kwamba bado hawajafanikiwa lakini wanafanya kila linalowezekana kuzuia vitu vya misimamo mikali kusambazwa katika kurasa zao.

Youtube inafanya nini kuwazuia watumiaji wenye msimamo mkali kusambaza imani zao?
kwa mujibu wa bandiko lililowekwa katika blog ya Google; Youtube inatarajia kuongeza wataalamu wanaojitegemea katika program yao ya kugundua video zinazo kiuka taratibu, pia kwa kutumia teknolojia ya kufananisha picha video zote ambazo zilipigwa marufuku (kipindi cha nyuma) zitakataa kupakiwa tena katika mtandao huo ili kuzuia video ambazo zilikwisha fungiwa kusambazwa tena.

Kama hiyo haitoshi mtandao huu umepanga kupanua makundi yake ambayo yanapambana na usambazwaji wa misimamo mikali, bandiko hilo limesema pia wataongeza msimamo juu ya video zote ambazo zina maoni yenye msimamo mkali.

Source:Teknokona

No comments:

Post a Comment

Pages