WHATSAPP NA MABORESHO MAPYA. - teknomovies
WHATSAPP NA MABORESHO MAPYA.

WHATSAPP NA MABORESHO MAPYA.

Share This
WhatsApp imeendelea kuonesha dhamira yake ya kubakia kuwa mtandao mkubwa zaidi katika mitandao ya kijamii, hili linadhihirika baada ya mtandao huo ambao unamilikiwa na Facebook kufanya majaribio ya Albamu za picha, filters na pia meseji za kufutika.

WhatsApp kuleta Albamu:
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za teknolojia
Techcrunch, toleo jipya la mtando huu linategemewa kuleta mambo mapya matatu kama ifuatavyo-:
Albamu za picha katika gumzo. Toleo jipya linalokuja linasemwa kwamba picha zaidi ya moja ambazo zinatumwa katika gumzo zitaunganishwa katika albamu moja ya picha, hii inategemewa kuondoa kero ya picha nyingi kuchukua nafasi ya sehemu ya gumzo.


Muonekano wa toleo jipya la Whatsapp lenye mabadiriko.
Imekuwa shida kwa muda mrefu kwa wapenda filters pale inapokuja app ya WhatsApp maana haikuwa na uwezo wa kurekebisha picha unazopiga ndani ya app hii. Kwa sasa watumiaji wataweza kuchagua kati ya filter tano ambazo zipo kwaajiri ya picha utakazo piga ndani ya app hii.
Meseji za kufutika.
Inasemekana kwamba Whatsapp wanataka kuleta uwezo wa mtu kufuta meseji picha gif ama video ambayo tayari umeishatuma, pengine hii ni moja kati ya vitu vya muhimu sana vilikuwa vinakosekana katika mtandao huu ( kumbuka msg mbali mbali unazokosea kutuma katika makundi).
Baada ya kupakua toleo jipya la Whatsapp na kulijaribu tumegundua kwamba huduma hii bado haijaachiwa lakini ni mategemeo yetu kwamba inakuja siku za usoni.
Kujibu meseji.
Mpaka sasa kama unataka kujibu meseji fulani katika mazungumzo ya WhatsApp inakubidi kubonyeza huo ujumbe kwa muda mpaka utakapopata menyu ambapo utachagua kujibu ujumbe, jambo hilo huchukua muda mrefu kidogo na pengine ndio maana wameleta njia fupi. Kwa sasa kujibu ujumbe utaswap tu katika ujumbe unaotaka kuujibu katika mazungumzo ama gumzo.
Kama tayari toleo hili jipya limekwisha kukufikia tuambie nini maoni yako juu ya maboresho hayo!


Chanzo:Teknokona
Mhariri : Frank Daxx

Pages