THE MENTALIST ANZA NAYO HAPA..!! - teknomovies
THE MENTALIST ANZA NAYO HAPA..!!

THE MENTALIST ANZA NAYO HAPA..!!

Share This
Yes, Huu mchongo rasmi ulianza kutoka kuanzia mwaka 2008 ikianzia mwezi September 23 na kumaliza mwezi February 18 mwaka 2015 ikiwa na mkusanyiko wa Episodes 151 Zikiwa Zimegawanywa Na Kukaa Katika Seasons 07.

Story kwa ufupi, inahusu jamaa anaitwa Patrick Jane ambaye alikua mtaalamu wa psychology mwanzo kabla hajajiunga na Kikosi maalumu cha uchunguzi wa issue za uhalifu.. Alifikia hiyo hatua baada ya mke wake na mtoto wake kuuwawa na jamaa aliyeitwa "Red John" ..na lengo la yeye kujiunga na polisi kuwasaidia katika Uchunguzi wa issue Mbalimbali za Uhalifu, ilikua ni kumtrack, huyo jamaa.

Patrick alikua anatumia uwezo wake wa psychology kugundua uhalifu, yani ni hivi, alikua ana uwezo akikuangalia unapojieleza anajua tu kua huyu anaongea uongo, huyu kweli or huyu sio... Pia kupitia uwezo huo alikua na uwezo wa kutumia njia za kijanja Mpaka ukajikuta unakili mwenyewe kosa...achana na hilo pia, alikua na ujuzi mkubwa katika kuchunguza hata eneo mauaji yalipofanyika na akahisi jinsi ilivyokua... Kuna akili kubwa sana alikua anatumia, and pia nilichokua nampendea ni jinsi anavyoongea.. Kama anacheka, afu hachekii Hivii...
Toeni, Blindspot sijui Nini Quantico. ... Kama unapenda series zile za watu na akili yao, hii hupaswi kukosa kuacha kuitizama, akili tu inatumika kuchambua mambo na si uchawi uchawi... Afu nimekumbuka Jamaa pia alikua mwizi hatari...


All in all Ukitaka kuanza kuucheki bonyeza HAPA utaona seasons zoote.. Utaamua mwenyewe ipi ianze.

Pages