The Keepers,Mzigo Mwingine Mkali Kutoka Netflix#Uchambuzi - teknomovies
The Keepers,Mzigo Mwingine Mkali Kutoka Netflix#Uchambuzi

The Keepers,Mzigo Mwingine Mkali Kutoka Netflix#Uchambuzi

Share This
Kama kawaida yao Netflix wazee wa kuachia michongo yote full, hawataki watu kuanza kusubiri sijui kila week Episode hiyo kwao hawana hata kidogo.

Nimetazama rates baadhi kwa mitandao mikubwa kama Imdb na Rotten Tomatoes ambapo kwa upande wa Imdb wao imekua rated 8.5 katika 10 na Rotten wao imekua rated 94% kwa asilimia 100%.

Kwa data hizo kidogo kabla hujatazama inaonesha kwa jinsi huu mchongo umepokelewa na watu, as you know hizo rate zinapigwa na watu.. Kabla hujaelewa vizuri hii Series ngoja nikupe Story kidogo.

Catherine Cesnic alikua ni nun(Monk wa kike) Ambaye alikua ni mwalimu pia katika shule ya wasichana iliyokua inamilikiwa na Kanisa hilo ikifahamika kwa jina la Archbishop Keogh High school huko Baltimore, Maryland.
Catherine Cesnic akiwa darasani kipindi cha uhai wake. 

November 6 mwaka 1969 alipotea katika mazingira ya kutatanisha ambapo mwili wake ulipatikana tayari akiwa kafariki January 03 mwaka 1970 ambapo mpaka leo chanzo hakikuwahi kufahamika lakini kwa vyanzo vya chini kwa chini vinasema kua chanzo inasemekana kua Kuna mapadre wawili mmoja aliitwa Joseph maskell ambao walikua wakiwafanyia unyanyasaji wa kingono wanafunzi wa shule hiyo.

Sasa Catherine inasemekana aligundua mchezo huo Mchafu ambapo alikua anataka kusema uchafu huo, lakini kabla ya hayo kutokea ndo kifo kikawa kimemtokea.

Hakuna Ushahidi wowote halisi ulionekana kuweza kushabiiana na Joseph maskell ambapo mpaka leo hakuna hata mtuhumiwa mmoja ambaye kawahi kufikishwa mahakamani kutokana na kesi hiyo.
Joseph maskell 

Hivyo basi Series hii, imetengenezwa ikihusiana na story nzima ya tukio zima.. Hakuna kilichopindishwa.

Unachokiona katika story nzima hiyo, ndivyo kilivyotokea katika Series pia.
Unaweza kupakua series hii, ambayo ina Episodes 07 tu.. Bofya HAPA

Pages