KIFAHAMU KITENGO MAALUM CHA (SPECIAL ACTIVITIES DIVISION) - teknomovies
KIFAHAMU KITENGO MAALUM CHA (SPECIAL ACTIVITIES DIVISION)

KIFAHAMU KITENGO MAALUM CHA (SPECIAL ACTIVITIES DIVISION)

Share This
(SAD) Special activities division ni kitengo maalumu kilichopo ndani ya shirika hilo la CIA.

Watu wanafahamu Umahiri na upekee wa shirika la CIA, lakini ndani ya CIA Kuna kikosi maalumu na cha kipekee,  kwaajili ya kazi nyeti na kazi hizo zinasimamiwa na maafisa wa Idara ya SAD, ndani ya CIA.

Yani kwa maneno mengine Idara ya SAD ilikua na maafisa wa kipekee ndani ya shirika la CIA.

UPEKEE WA (SAD) NDANI YA (CIA) NI  NINI?

Kutokana na kuongezeka kwa changamoto za kimataifa, ambazo zingine zinatishia usalama au maslahi ya marekani ,ambayo marekani haiwezi kuchukua hatua zozote kutokana na kujiepusha na lawama kutoka kwa Jamii ya kimataifa, Ndipo hapo ikaonekana Kuna Umuhimu kuwa na kitengo maalum kwajili ya swala hili.

Ndipo hapo serikali ya marekani ikaagiza shilika la ujasusi la CIA kuanzisha kitengo maalum ndani yake ambacho kitakua na maafisa (wanajeshi) ambao wanaweza kutekeleza opresheni yoyote ya kijeshi kwa kujitegemea, pasipo kuhusisha serikali ya marekani.

CIA wakaanzisha Idara maalumu ndani yake na kuiita (special activities division) au kwa kifupi (SAD) ambayo ilikua na maafisa wa siri ambao hawabebi vitambulisho na majina yao ni Siri hawawezi kupatikana hata kwenye orodha ya maafisa wa CIA.

Lengo hasa la kuanzisha kitengo hiki ni kutekeleza oparesheni maalum za kijeshi au propaganda na ikitokea wakakamatwa au kushtukiwa basi serikali ya marekani inawakana kuwa si maafisa Wao, (plausible deniability).
Kwahiyo kitengo hiki kinafanya kazi kwaniaba ya serikali ya marekani lakini hakuna uwezekano wowote wa adui kuunganisha uhusika wa kikosi hiki na serikali ya marekani .

Kitengo cha kwanza kinaitwa (political action group) kitengo hiki kazi yake kubwa ni kufanya ushawishi wa kisiasa (political in fluence) oparesheni ya kiuchumi (Economic warfares) pia kutokana na Maendeleo ya ki teknolojia kitengo hiki kimeongezwa jukumu la vita ya kimtandao, (cyberwarfares).

Tuchukulie kwa mfano Kuna nchi fulani Kuna serikali au mwenendo wa serikali unatishia Maslahi ya marekani, basi kitengo hiki kinaingia kwa Siri kubwa Sana na kufanya moja wapo ya mambo ambayo nimeorodhesha hapo juu.

Moja wapo ya matukio ambayo kikosi hiki kimehusika Sana na CIA wamekiri kwa nyalaka zilizo wekwa wazi mwaka (2004) ilikuwa ni kueneza propaganda ambayo ilichangia kupinduliwa kwa Rais wa Iran mwaka (1953).

Pia kitengo hiki kilitumika kuzuia chama cha ki komunisti cha Italy kushinda uchaguzi mwaka (1960).
Pia kitengo hiki kimewahi kufanya oparesheni ya Siri iliyoitwa (operation mockingbird) katika taifa la marekani oparesheni hii ilikua na lengo la ku control habari zilizoandikwa na vyombo vya habari nchini humo.

Kitengo cha pili kinaitwa (special operations group) kifupi ( SAG) na kazi yake ni kama ifuatavyo:
Kitengo hiki kinajumuisha wanajeshi wenye weledi wa juu kutekeleza malengo ya kivita pasipo kujulikana kwa uhusika wa serikali ya marekani.
Ili Kulinda utambulisho Wao wanajeshi wa kikosi hiki maalum hawavai sare za jeshi wala kubeba kitambulisho .

Inasemekana hiki ndo kikosi maalum cha oparesheni za kijeshi chenye usili mkubwa sana kwa Marekani.


Mwandishi : Amanyisye Ulimboka.
Mhariri : Frank Daxx.

Pages