MZIGO MWINGINE TENA, TOKA KWA CHRIS BROWN UNAKUJA. - teknomovies
MZIGO MWINGINE TENA, TOKA KWA CHRIS BROWN UNAKUJA.

MZIGO MWINGINE TENA, TOKA KWA CHRIS BROWN UNAKUJA.

Share This
Tumeona watu Mbalimbali maarufu wakitengenezewa na wengine kutengeneza Documentary Mbalimbali ambazo zinahusu maisha yao mfano kama Serena Williams, Christiano Ronaldo, Usain Bolt ni Baadhi ya Watu maarufu duniani walioamua kuweka Story zao katika mtiririko wa movie.
June 8 ambayo itakua ni Alhamisi, ni siku ambayo itakua ya kipekee pia kwa msanii maarufu kutokea pande za marekani Chris Brown ambapo Documentary yake inayokwenda kwa jina la Chris Brown : Welcome to My Life ndo siku itayokua inaachiwa kwa mara ya kwanza.

Katika Documentary hiyo, utapata kuona story yake nzima mpaka kuja kua super star anaefahamika dunia nzima mambo mangapi alipitia kabla ajafikia level hii anayoonekana sasa.
Katika Documentary hiyo utaona mambo Mbalimbali, kama shows zake, behind the scenes za studio na mazoezini na zaidi utaziona sura hizi katika mchongo huu kama Jamie Foxx, Dj Khaled, Usher Raymond, Justin Bieber, Jennifer Lopez na Wengineo wengi tu.
Hakika ni Documentary ambayo haitakiwi kuikosa ndugu yangu, Team yetu ikiupata tu mchongo haraka utasababishwa hapa.
Unaweza ukaacha maoni yako hapo chini kuhusu hichi kitu.

Pages