UNAMJUA JAMES WAN WEWE? MKALI NYUMA YA HORRORS - teknomovies
UNAMJUA JAMES WAN WEWE? MKALI NYUMA YA HORRORS

UNAMJUA JAMES WAN WEWE? MKALI NYUMA YA HORRORS

Share This
Huwa tunawazungumzia mastar Mbalimbali wa movies na series pia, lakini tunawasahau watu ambao hufanya kazi nzito sana kuzidi hata hao waigizaji.

Katika uandaaji wa movie, kwa wenzetu kuna kua na composition ya watu wengi sana sana, ambao wengine hupewa credit lakini wengine hawapewi credit lakini kazi yao huwa ni nzito lakini ndo hivyo humezwa na waigizaji.

Katika picha unamuona jamaa huyo ambaye kwa jina anafahamika sana kwa jina la JAMES WAN, and yes ndo jina lake halisi Ambalo utalipata vilivyo katika passports zake zote.

Tarehe yake ya kuzaliwa ni tarehe 27 February mwaka 1977,na alizaliwa huko malaysia lakini ana uraia wa australia.

Kabla hajafanikiwa kwa kiasi kikubwa, aliandaa filamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Stygian " akiwa pamoja na shannon young wakishirikiana katika uandaaji, movie hiyo ndiyo iliyofungua baraka, kwani walifanikiwa kushinda tuzo kama "Best Guirella film" katika Melbourne underground Film Festival " hiyo ilikua mwaka 2000.

Mwaka 2001 Akiwa pamoja na rafiki yake Leigh Whannel waliandika kwa pamoja filamu ya kutisha yote ikiwa influenced na jinsi wao vitu wanavyoviogopa na pia ndoto za kutisha, hiyo filamu wengi wenu mnaijua kama SAW... Lakini Nchini Australia Idea yao hiyo ilikataliwa katika makampuni ya movies wakiona kama haitakua na faida, ambapo waliamua kusafiri kwenda Los Angeles California ,Marekani lengo ni kutafuta kampuni kuwadhamini. Ila unajua walifanyaje ili kushawishi hayo makampuni??

Waliamua kushoot filamu fupi isiyo na script ikiwa na jina hilo hilo la SAW kwa budget ndogo jambo ambalo lilifanikiwa kuwashawishi ambapo kufikia mwaka 2003 kazi kazi ikaanza ambapo Evolution Entertainment waliamua kuishoot Serious, na ikitumia budget ndogo kabisa ya $1.5M lakini kimauzo Ilifika mpaka $100M na kuifanya kua Filamu Ya kutisha iliyouza zaidi Ikiipiku filamu ya scream ya mwaka 1996. Ila kwa marekani ni filamu ya pili ikiachwa na Friday the 13th nights films kwa $10M.

Baada ya mafanikio hayo, ndipo SAW ilizidi Kuachiwa huku kwa pamoja na Whannel wakishiriki kwa kiasi kikubwa kuiandaa, lakini sio kazi hiyo tu ambayo mtu mzima James katia mikono yake... Kuna kazi nyingi sana na kali kazipitisha katika ubongo wake na kumfanya kua Mojawapo ya waandaji wa movies makini kabisa...

Tukianza Na Hii DEATH SENTENCE " ambayo ilitoka mwaka 2007. Hii movie haikua ya kutisha ila ilikua ikielezea story kumuhusu Baba aliyeamua kulipiza kisasi baada ya mtoto wake kuuliwa na kundi la wahuni.

Filamu ya Tatu Kufanya kazi tena ilikwenda Kwa Jina La INSIDIOUS iliyotoka mwaka 2010 nayo ikiwa ya kutisha pia ambapo sokoni ilifanya vyema sana kutoka budget ya $1.5M mpaka kuuza $97M Na kupelekea kutoka nyingine zaidi zaidi .

Sio hiyo michongo tu ambayo alifanya kazi vilivyo, Nani asieijua FAST AND FURIOUS 7??. Movie bora kabisa iliyotoka mwaka 2015 ambayo ilizidi zaidi kuonesha ubora wake kwa kutumia budget ya $190M na kuuza $1.5B

Sio Hizo tu, vipi kuhusu THE CONJURING? LIGHTS OUT,ANNABELE....Ni baadhi ya vyuma vikali sana alivyofanya huyu mtu.

Na sasa Jiandae na mizigo miwili ya nguvu, THE INSIDIOUS CHAPTER 4 itayotoka OCTOBER 20 na SAW:LEGACY itayotoka October 27.



No comments:

Post a Comment

Pages