STEVEN Kanumba alizaliwa huko Shinyanga tarehe 8 Januari mwaka 1984.
Baba yake aliitwa Charles Kanumba na mama yake Flora Mutegoa. Kanumba alikuwa na dada zake wakubwa wawili. Alianza shule katika shule ya msingi ya Bugoyi , kisha akaendelea na masomo ya sekondari Mwadui Secondary School, na baade kuhamia Vosa Mission Secondary School.
Kanumba alianza shughuli za sanaa katika miaka ya 90 kwa kushiriki katika michezo ya kuigiza ya kanisani, na mwaka 2002 akajiunga na kundi la Kaole Arts Group. Akaanza kuonekana kwenye tamthiliya za kikundi hicho kama vile Jahazi na Dira.
Filamu yake ya kwanza ilikuwa ni Haviliki. Mwaka 2006 akakutana na Nazz aliyemuunganisha katika kuweza kushiriki katika filamu ya Mtitu Game iliyoitwa, Dar 2 Lagos, filamu iliyochanganya wasanii kutoka Tanzania na Nigeria.
Katika mtiririko huo akashiriki katika filamu kama She is My Sister, This Is It na Love Gamble.
Mwaka 2009 akawa mmoja wa ’celebrity guest’ kwenye onyesho la Big Brother Africa 4. Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Oxfam GROW. Tarehe 7 April 2012 habari zilianza kusambaa kuwa Kanumba amefariki, baadae ilikuja kujulikana kifo kilitokana na kujigonga au kugongwa na kitu kizito kichwani wakati akiwa na mpenzi wake Elizabeth “Lulu” Michael Kimemeta.
Lulu hatimae alifunguliwa mashtaka kwa kifo hicho. Msiba wa Kanumba ulikuwa mmoja wa misiba iliyoutingisha mji wa Dar es Salaam kuna watu husema watu 25,000 walihudhuria shughuli za kuaaga na kumzika marehemu ambaye alizikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Steven Kanumba alifanya kazi kubwa katika tasnia ya filamu kati ya tuzo alizoshinda ni;
*.2006 Best Actor of the Year
*.2007 Best Actor in Tanzania Award
*.2007/2008 Best Artist of the Year Award
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.
No comments:
Post a Comment