BILIONEA ROCKEFELLER AFARIKI DUNIA. - teknomovies
BILIONEA ROCKEFELLER AFARIKI DUNIA.

BILIONEA ROCKEFELLER AFARIKI DUNIA.

Share This
Taarifa ikufikie kuwa aliyekuwa mkurugenzi wa Kampuni kubwa ya mafuta nchini Marekani David Rockefeller amefariki dunia tarehe 20 march akiwa na umri wa miaka 101.




David alikuwa mjukuu wa mwisho aliyekuwa hai wa Muanzilishi mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Tycoon Oil John. D. Rockefeller nembo halisi ya New York.


David Rockefeller amefariki akiwa nyumbani kwake Pocantico Hills, New York baada ya kuugua kwa muda tu alipopata shambulizi la Moyo. Daktari wake amethibitisha.

Amefariki akiwa amelala. David alikuwa mjukuu wa John Rockefeller bilionea wa kwanza Marekani ambae alikuwa muanzilishi wa kampuni ya mafuta ya Standard Oil and the United State.

David amefariki akiwa ameshikilia rekodi ya bilionea mzee zaidi Marekani.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi Ameen.

No comments:

Post a Comment

Pages