Pombe inayotokana na mkojo wa binadamu! #Teknolojia - teknomovies
Pombe inayotokana na mkojo wa binadamu! #Teknolojia

Pombe inayotokana na mkojo wa binadamu! #Teknolojia

Share This
Wengi wanaamini kuwa mkojo ni dawa lakini fikiria sasa mkojo utumike kutengenezea pombe, utakuwa tayari kuinywa pombe hiyo?

Katika hali ya kuwa na pombe zilizotokana na vimea mbalimbali ni dhahiri kuwa mkojo wa binadamu umekuwa mstari wa mbele kutumiwa katika utengenezaji wa pombe na nchini Denmark Kiwanda kimoja cha pombe kimetengeneza bia mpya kwa kutumia shayiri ambayo imekuzwa kwa kutumia lita 50,000 za mkojo .
Sehemu inapochanganywa
Mkojo huo ulikusanywa kutoka tamasha ya Roskilde ambayo ndiyo hafla kubwa zaidi ya muziki Ulaya kaskazini miaka miwili iliyopita.

Pombe hiyo imeonekana kuvutia watu mbalimbali na mmja ya wanywaji wa pombe hiyo inayotokana na mkojo alithubutu kusema kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi .
Ingawa pombe hiyo inatengenezwa lakini baraza la chakula la nchini Denmark limetoa ushauri wa kutumiwa kwa mkojo kama mbolea ya kurutubisha shayiri ambayo baadaye inatumiwa kutengeneza pombe .
Wakati bia hiyo inaanza kutengenezwa watu walidhani kampuni inayotengeeneza bia hiyo walikuwa wanaweka mkojo moja kwa moja baada ya bia hiyo kutengenezwa lakini bada ya muda walikuja kuelewa si vile walivyokwa wanavyofikiria.

Kampuni ya Norrebro Bryghus inayomiliki kiwanda hicho hata hivyo imesema bia hiyo haitakuwa na masalio yoyote ya mkojo wa binadamu.

Je, bia hiyo ikiletwa huku kwetu utakuwa tayari kwa kunywa?

Source: Teknokona pamoja na Picha.

Pages